Ajali ya Lori na Bajaji yaua wanne Mafinga

Ajali ya Lori na Bajaji yaua wanne Mafinga

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Watu wanne wamefariki dunia baada ya lori kugongana na Bajaj katika eneo la Kinyanambo- Mafinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji Mafinga, Dk Victor Msafiri amesema ajali hiyo ilitokea jana usiku.

Dk Msafiri amesema walipokea miili ya wanaume wawili, mwanamke mmoja na mtoto mmoja. Amesema kuwa hadi sasa mwili mmoja tayari umeshatambuliwa na ndugu kwa ajili ya kuendelea na taratibu zingine za mazishi huku miili mingine ikiwa bado imehifadhiwa katika hospitali hiyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Issa Juma Suleiman amesema chanzo cha ajali hiyo ni uendeshaji usiozingatia sheria za usalama barabarani. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Madereva Bajaj Mafinga Mjini, Aroun Manga amesema walipokea taarifa kwamba kuna ajili maeneo ya Kinyanambo.

"Ni kweli tulifikia hadi eneo la tukio tulikuta bajaji ikiwa imelaliwa na lori tulipojaribu kuitoa tulikuta watu wote wamepoteza maisha akiwa na dereva wetu ila kwa sasa tupo njia tunaelekea Songea kwa ajili ya kumpunzisha dereva mwenzetu katika nyumba yake ya milele" amema Manga

Pia ameeleza kuwa mji wa Mafinga umekuwa na msongamano mkubwa wa vyombo vya moto hivyo kuiomba Serikali kuangalia namna bora ya kujenga barabara za pembeni ili bajaji ziweze kupita katika njia hizo.

"Mfano nzuri kwa wenzetu wa mji wa Makambako wamejengewa barabara za pembeni ndio ambazo wanazitumia hivyo tunaiomba Serikali kutujengea barabara hizo ili kupunguza ajili na kuokoa maisha ya abiria na madereva Bajaj katika Mji wetu." amesema Manga

MWANANCHI
 
Hizi bajaji za manzese ,,Mbezi zinaua kila siku lakini wenye sirikali kimya!!! Poleni wafiwa
 
Bajaji na bodaboda, madereva wa hivi vyombo huwa hawapo makini kabisa. Wao wakijua kuendesha tu basi, habari za sheria za barabarani sio zao. Na huko tunakokwenda vyombo hivi vitakuwa kama utitiri barabarani, kwa hivyo tutegemee ajali nyingi zaidi.
 
Bajaji na Bodaboda TOYO na Powertiller wengi wao huwa hawafuati sheria za Barabarani.

Utasema wanaendesha Vifaru kwamba ukimgonga unaumia wewe.
Hawa watu nina negative feelings nao sana. Naomba tu isitokee nikawanyima haki pale wanapostahili kwendana na negativity juu yao.
 
Kuna VIFO SIO MIPANGO YA MUNGU bali vinatokana na MIPANGO MIBOVU ya WASOMI wetu uchwara.

Fikiria Jiji la Daaslam tulipiga stop HIACE tukaziita Vipanya halafu leo tumeruhusu BAJAJ Utitiri?
Unajiuliza ni Akili au ni Bangi?

Highway Unaruhusu Bajaj ni akili au ni UTI imekula Ubongo? Kwa kifupi akili ya Mtu mweusi akina sisi ina Mapungufu ya kimaumbile ndio maaana Sheria na Matendo yetu Vinachekesha na kutia Simannzi.

Kwa kifupi BAJAJ na BODABODA hazipaswi kuwepo Katikati ya Majiji na kwenye HIGHWAY.

Period
 
Bajaji na bodaboda, madereva wa hivi vyombo huwa hawapo makini kabisa. Wao wakijua kuendesha tu basi, habari za sheria za barabarani sio zao. Na huko tunakokwenda vyombo hivi vitakuwa kama utitiri barabarani, kwa hivyo tutegemee ajali nyingi zaidi.
Bodaboda, yupo nyuma ya gari yako, upande wa kushoto, na anataka apinde kulia.
badala ya kuomba gari, iliyo nyuma yake, anaenda kupinda mbele ya gari yoko gafla tu.
 
Kuna VIFO SIO MIPANGO YA MUNGU bali vinatokana na MIPANGO MIBOVU ya WASOMI wetu uchwara.
Fikiria Jiji la Daaslam tulipiga stop HIACE tukaziita Vipanya halafu leo tumeruhusu BAJAJ Utitiri??
Unajiuliza ni Akili au ni Bangi?
Highway Unaruhusu Bajaj ni akili au ni UTI imekula Ubongo?? Kwa kifupi akili ya Mtu mweusi akina sisi ina Mapungufu ya kimaumbile ndio maaana Sheria na Matendo yetu Vinachekesha na kutia Simannzi.
Kwa kifupi BAJAJ na BODABODA hazipaswi kuwepo Katikati ya Majiji na kwenye HIGHWAY... Period
Eti, zimeondolewa hiace, kwa sababu ya msongomano, wameingiza bajaji.
 
Mara nyingine unaendesha Semi lina tani 32 wanakupigia honi uwapishe😁

umenikumbusha, kuna boya mmoja Magomeni, semi lilipita kwa spidi, likamrushia yule boda Maji ya dimbwi yaliyokua barabarani pembezoni

boda kawasha chuma kaanza kuikimbiza semi, akaidaka karibia na bakhressa akawa anapiga pembeni ili mwenye Semi asimame

mwenye semi kampelekea kule kule alipo, iliyopona ni pikipiki tu, jamaa yuko kwenye tairi za nyuma zile mbili zinazokaa pamoja kasagika vibaya mno aka RIP hapohapo
 
Dereva wa Semi Shujaa
 
Back
Top Bottom