je hii itasaidia kwa upande wa barabara au miradi wa wakubwa kama ilivyokuwa speed gavana
Wamiliki mabasi wapewa miezi mitatu kufunga kidhibiti mwendo
Saturday, 21 May 2011 09:47
Mwandishi Wetu, Morogoro
KAMANDA wa Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga, ametoa miezi mitatu kwa wamiliki wa mabasi kufunga kifaa cha mfumo wa kuonyesha mwenendo magari.
Pia, ameagiza makamanda wa mikoa wa usalama barabarani nchini kutohuisha leseni za usafirishaji au kutoa mpya kwa magari ambayo hayajafunga kifaa hicho.
Mpinga alisema muda huo unaishia Agosti mwaka huu, umetolewa kutokana na wamiliki wengi kulalamika kwamba hawajapata elimu ya mfumo huo unavyofanya kazi na gharama zake.
Akizungumza kwenye maonyesho kwa kamanda wa usalama barabarani nchini na maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra) juzi, Kamanda Mpinga alisema hata waliofunga licha ya kubainika kukiuka sheria za barabarani, hawajaanza kuwachukulia hatua.
"Hivi sasa hatujaanza kuchukua hatua hata kwa wale waliofunga, bali tunachofanya ni kuwapigia simu tunapobaini kwenye mfumo kuwa wanakwenda kasi, kwa sababu tulitarajia awamu ya kwanza kufunga mabasi 500, lakini hadi sasa ni 48 pekee yaliyofunga," alisema.
Kamanda Mpinga alisema kufungwa kwa kifaa hicho kunakofanywa na Kampuni ya Utrack Africa Ltd, kutapunguza kwa kiwango kikubwa ajali ambazo zimekuwa zikitokea.
Aliendelea kuwa kifaa hicho ambacho pia kina kamera kitasaidia polisi na wamiliki, kwa sababu anaweza kuona abiria waliopo kwenye basi lake muda wowote.
Pia, Mpinga alisema hivi sasa anafanya mawasiliana ili serikali isimamie mradi huo, badala ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (Taboa), kwa sababu una manufaa zaidi.
Akitoa maelezo jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi, Mkurugenzi Mkuu wa Utrack Africa Ltd, Zulfikar Mohamed, alisema mifumo yao siyo tu kwa ajili ya kurekodi mwendo kasi kwenye mabasi, bali pia una faida nyingi kwa wamiliki.
Mohamed alisema mmiliki anaweza kufuatilia tabia za uendeshaji wa madereva wanapokuwa safarini, taarifa za safari, kamera za kupiga picha ili kujua idadi ya watu waliopo ndani ya basi na kwa maslahi yake kujua idadi ya abiria na usalama pale linapotokea tukio la uhalifu.
Pia, alisema mfumo huu unatumiwa na wenye malori ya mizigo na mafuta, kampuni za wawindaji, kampuni za utalii, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's) , kampuni za kutengeneza barabara, madini na kampuni binafsi zinazofanya biashara mbalimbali.
NILIPOKUWA UK hakuna upuuzi huu ila kila gari inafuata ratiba na hivyo kuzibiti mwenzo, wanakamela mabarabraba lakini sisi tukiweka ratiba ni njia bora zaidi,
ratiba ya gari ndio kipimo kizuri, kwa nini kila stand kubwa ya mabusi kusiwe na kituo cha trafic wanaoweza kuratibu ratiba ya mabasi kwa kutumia ratiba?
kama basi litafika mapema ya muda wanapigwa fine
mimi nadhani hii inaweza kuwa bora zaidi kama wao polisi watatumia mfumo ya pc kujua basi linaingia na kuondoka saa ngapi kwenye kila kituo kuliko haya maduu wanayoweka