Ajali ya ndege imetokea jimbo la Florida na kusababisha vifo vya watu 9

Ajali ya ndege imetokea jimbo la Florida na kusababisha vifo vya watu 9

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Watu tisa waliokuwa wamesafiri na ndege wamefariki dunia baada ya ndege hiyo kuanguka karibu na eneo la makazi katika Kaunti ya Palm Beach, jimbo la Florida, nchini Marekani, siku ya Jumapili mchana.

Kwa mujibu wa Waziri wa Uchukuzi wa Marekani, Sean Duffy, ndege hiyo ilianguka na kuua abiria wote waliokuwa ndani kabla ya kushika moto na kulipuka.

Ajali hiyo inatajwa kuwa ya pili kwa kusababisha vifo vingi zaidi nchini Marekani mwaka huu, kwa mujibu wa rekodi za Bodi ya Taifa ya Usalama wa Usafirishaji (NTSB).

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) imesema ndege iliyopata ajali hiyo ilikuwa aina ya Learjet 60, iliyokuwa ikielekea nchini Bahamas kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Austin-Bergstrom.

Kwa mujibu wa rekodi za FAA, ndege hiyo imesajiliwa kwa kampuni yenye ukomo wa dhima (LLC) iliyoko katika jimbo la Delaware, huku pia ikitajwa kuwa ilikuwa ikipatikana kwa huduma za kukodi ndege.

FAA na Bodi ya Taifa ya Usalama wa Usafirishaji (NTSB) zinatarajiwa kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo na mazingira ya ajali hiyo.
=================
A plane carrying nine people crashed near a residential area and killed all the passengers on board before erupting in a fireball in Palm Beach County, Florida, on Sunday afternoon, Transportation Secretary Sean Duffy said on X.

The crash is the second deadliest in the United States this year, according to NTSB records, following June's skydiving plane crash in Butler, Missouri, which killed 12.

The plane was a Learjet 60 flying to the Bahamas from Austin-Bergstrom International Airport, according to the Federal Aviation Administration. It is registered to an LLC in Delaware, according to FAA records, and is listed as available for charter online.

The FAA and National Transportation Safety Board will investigate the crash, the FAA said.















​
 
Back
Top Bottom