Ajali za barabarani zimezidi kupoteza Maisha ya Watanzania. Hatua madhubuti zichukuliwe kudhibiti

Ajali za barabarani zimezidi kupoteza Maisha ya Watanzania. Hatua madhubuti zichukuliwe kudhibiti

F4B

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2022
Posts
336
Reaction score
429
Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan naomba kukuomba uchukue hatua madhubuti na za makusudi katika kudhibiti ajali za barabarani hapa nchini kwani zimekuwa zikigharimu Maisha ya watanzania. Leo Mbeya, Sengerema , juzi juzi hapa watoto wa shule huko Mtwara.

Ningependa kuona sheria zetu za barabarani zikifanyiwe MAREKEBISHO. Mhe Rais chukua hatua lkn wahusika pia chukueni hatua za kuwajibika.
 
Tz matukio ya ajali yanapotokea ndiyo utaona maafisa usalama barabarani na vitambi vyao na mbwembwe kibaao kwa ushauri wangu ushauri wa Kinana Upuuzwe
 
SISI KAMA MATRAFIKI TUNAKUFA NA NJAA MAMA TUONEE HURUMA TURUDI BARABARANI.
 
Cha msingi zaidi ni kuboresha miundombinu vizuri, haiwezekani barabara kama ya mbeya kila siku kuna nyuzi watu wnalalamikia serikali madimbwi, vilaka na uchakavu kwa ujumla wa barabara

Sasa kama Serikali inashindwaje kueeka bajeti nzuri na kutanua barabara hata njia mbili kwenda na mbili kurudi kwa usalama wa raia, tunapoteza raia kizembe

Pia sheria kali kwa wavunja sheria hasa watumiaji vyombo vya moto na ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vyote
 
Kwanza waanze na ubovu na uduni wa barabara. Highway iwe highway kweli, sasa barabara ya Dar - Mbeya, Ar, KLM, Dom n.k ni kama vichochoro vya Ilala.

Weka angalau lane mbili upande mmoja, lane mbili upande wa pili.

Ikitokea bahati mbaya, ajali iwe ya kutoka nje ya barabara na sio H2H collision. Kona kona za kifala zife, ingawa kusikia ajali imetokea Sekenke au Kitonga sijui mara ya mwisho ni lini!
 
Mbona miaka 6 iliyopita ajali zilipungua sana.kwani speed 50 haifuatwi tena? Maana hizi ajali ni too much sasa.ukizingatia na barabara zetu zilivyo hovyo.
 
Weka mapendekezo yako mkuu.
Mapendekezo yangu barabara ziboreshwe, vyombo vya usafiri vikaguliwe mara kwa mara na mwisho madereva waongeze umakini wanapokuwa wanaendesha magari.
 
mabandiko haya yooote ya polisi wanalazimisha kurudishwa barabarani, kana kwamba kabla ya wao kupunguzwa huko road ajali zilikua hazipo, shame on them tafuteni kazi nyingine hela mlizokua mnajichukulia za rushwa sasa baaaasi Kinanan JUUUUUUUU, inawezekanaje umbali kama Dar Morogoro mtu unatumia masaa 6 ni maendeleo gani hayo mnataka
 
mabandiko haya yooote ya polisi wanalazimisha kurudishwa barabarani, kana kwamba kabla ya wao kupunguzwa huko road ajali zilikua hazipo, shame on them tafuteni kazi nyingine hela mlizokua mnajichukulia za rushwa sasa baaaasi Kinanan JUUUUUUUU, inawezekanaje umbali kama Dar Morogoro mtu unatumia masaa 6 ni maendeleo gani hayo mnataka
Wanataka Waendelee kuchukua rushwa
 
Kila kitu Raisi atusaidie Raisi atusaidie sijui ni IQ zetu za kuvukia Barabara au ni laana fulani.

Halafu unamkuta kwenye Basi liko spidi ya kutoa Roho eidha kasinzia au anakula mua.
 
Back
Top Bottom