Ajali za magari kugonga treni zinaongezeka. Wizara zinazohusika zichukue hatua

Ajali za magari kugonga treni zinaongezeka. Wizara zinazohusika zichukue hatua

budagala

Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
75
Reaction score
137
Kwa utafiti wangu kiasi, kuna uelewa mdogo wa watumiaji wa vyombo vya usafiri wanapokaribia maeneo ambayo gari moshi hupita. Inawezekana baadhi yao hawana elimu ya mvutano wa vyombo vyao vinapokaribia gari moshi.

Lakini pia Taasisi zote zinazohusika ikiwemo jeshi la polisi usalama barabarani, watoe elimu kwa umma (vipindi vya luning) juu ya kinachoweza kutokea vyombo vya moto vinapokaribia treni. Ikiwezekana itumike hata teknolojia ya boom gate kujifunga endapo treni inapita.

Ajali na vifo vya aina hii vinaongezeka sana japokuwa naamini tunaweza kuvipunguza au kuviondoa kabisa.
 
Treni ya mwendokasi SGR Itaua zaidi🤣🤣🤣🤣🪑
 
Dharau za madereva wa magari tu. Anakadiria mwendokasi wa treni kwa kufananishia na mwendo wa Bajaj.
 
Madeva wengine ni walevi tu, wanaona reli inakatiza mbele lakini anavuka bila kusimama kwanza ajiridhishe kama kuna treni au hata kiberenge ndio avuke yeye anaona anachelewa anavuka kibishi tu, mazoea mabaya, siku nyingine anavuka bila kusimama kumbe treni nayo hii hapa anaigonga na matokeo yake ni ajali.
 
Hata ukienda huko TRC wakupe number ya train accidents, fatalities, maeneo gani ajali zinatokea sana. Etc with data ili policy advisor wapate picha ya ukubwa wa tatizo, kama kuna ulazima wa intervention na wapendekeze hatua gani za kupunguza tatizo, TRC na TAZATA hizo data hawana.

Ni nchi inayoendeshwa kwa kudra za mungu.

Halafu tunataka train za 160km/ph salaleeh
 
Ukweli ni kwamba Tanzania au Tanganyika tunaongozwa na sheria zilizopitwa na wakati. Twende kwa wenzetu Ulaya, tujifunze sheria za reli onapokatisha barabara kuu. Maneno kwamba dreva wa gari kagonga treni waliyafuta zamani, sisi tumebaki kukariri ili shirika la reli lisiwajibike.

Imeundwa beriya inayofunga barabara automatic kila treni au kibelenge kikikaribia mita 100, kabla ya kivuko cha barabara, pia kengere zinalia kea nguvu mithili ya kanisani.

Wajibu wa dreva wa gari ni kuwa makini na hizo ishara na ajue zinaweza kushindwa kufanya kazi kwa hujuma au hitilafu. Gharama ya kuweka automatic moja kwenye kivuko ni usd 2000 saws na sh 5m.
Tujiulize kea nini Trc inashindwa kuleta huo mpango?

Vipi SGR imeelekezwa huo mfumo? Naomba wabunge wetu wakialikwa kutembelea huo mradi wa SGR waulize hilo swali? Bado hatujachelewa. Ni vizuri wale wanaotembea nchi za nje wakirudi kwetu washauli mambo gani yamepitwa na tekinolojia. Hakuna tena gari kugonga treni kwa wenzetu.
 
Nasikia kuna dc huko chamwino naye kayatimba wameparamia bichwa la treni

Ova
 
Middle class lini mtaanza kufikirisha akili?,hakuna kitu kinachoitwa umegonga treni huu ni upumbavu tuliorithishwa!,uzembe wa mamlaka husika kuzuia hizi ajali ndio tatizo, why hadi leo tuna vivuko vingi vinavyoingiliana, ilitakiwa kimoja lazima kichepushwe, na inapokua imeshindikana kuchepusha basi ni muhimu mno alama ziwekwe za kuzuia hizi ajali, na Drivers PLEASE SIMAMA kwenye rail crossing hata kama rail haitumiki
 
Kwa utafiti wangu kiasi, kuna uelewa mdogo wa watumiaji wa vyombo vya usafiri wanapokaribia maeneo ambayo gari moshi hupita. Inawezekana baadhi yao hawana elimu ya mvutano wa vyombo vyao vinapokaribia gari moshi.

Lakini pia Taasisi zote zinazohusika ikiwemo jeshi la polisi usalama barabarani, watoe elimu kwa umma (vipindi vya luning) juu ya kinachoweza kutokea vyombo vya moto vinapokaribia treni. Ikiwezekana itumike hata teknolojia ya boom gate kujifunga endapo treni inapita.

Ajali na vifo vya aina hii vinaongezeka sana japokuwa naamini tunaweza kuvipunguza au kuviondoa kabisa.
🤣🤣🤣🤣🤣

View: https://www.instagram.com/p/C0RGA7ONlFw/?igshid=NmJiYWZiY2E0Mg==
 
Treni ya mwendokasi SGR Itaua zaidi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]🪑

SGR haitakuwa na Sehemu ambayo Barabara Inakutana na Reli, ndio maana sehemu zote ambazo reli inakutana na barabara kuna aidha daraja au andaki.!
 
Binadamu wote, Iwe Muhindi, Mwafrika, Mzungu , Muasia , au Kabila lolote .ni binadamu anayehitaji VIKWAZO .

Kila palipo na HARUFU ya hatari weka KIKWAZO kama ni barabarani weka TUTA ashindwe kupita bila Tahadhali.

Traffic ni kikwazo lakin baada ya muda kinaondoka weka TUTA maana hili hata HONI halisikii, rushwa halichukui na halina mzaha.
 
Mambo ni magumu kwa kweli,watu wanakufa kama sisimizi
 
Back
Top Bottom