Mkuu kunaweza kuwa na sababu nyingi tuu. Mojawapo Vodacom ni kampuni kubwa na maarufu sana Tanzania, so watu wanafikiri it should lead by examples. Nafikiri kati ya hao sponsors watano, Vodacom ilikuwa ndio kampuni kubwa. Sababu nyingine Vodacom imekuwa sana mstari wa mbele ku champion corporate social responsibility. Kwa sababu hii tuu yenyewe watu wengi wanadhani Vodacom ingekuwa mstari wa mbele kama walivyokuwa kwenye mabomu ya gongo la mboto. Kumbuka hii coporate social responsibility ni mojawapo ya sababu inayoifanya vodacom kulipa kodi ndogo zaidi ya Airtel japokuwa vodacom ina wateja wengi zaidi ya Airtel. Watu wanauliza where was vodacom corporate social responsibility kwenye hili janga?

Wapo wengine wanasema Vodacom haina wateja wengi Zanzibar ndio sababu waliamua kuendelea na Miss Tanzania. Sidhani hata vodacom wataikubali hii sababu b'se kibiashara haijakaa vizuri. Vipi kama janga lilikuwa limetokea Tanzania bara? Unafikiri haya mashandano yangeendelea? This event was not Miss Tanzania Mainland. It was Miss Tanzania. Kama alivyosema Mh Zitto hili janga lime test umoja na utu wetu. Kwa hili janga tumejua umoja, ushirikiano na utu wetu upo wapi.

Ku sponsor tuu Miss Tanzania itself ni corporate social responsibility. Pia kwa kampuni kusaidia watu watu waliokubwa na janga ni part ya corporate social responsibility. Na haya mambo yanapotokea kwa wakati mmoja inaweza kuwa ngumu ku make a right decision. But as a company, you will have to make a bold decision. Na katika maamuzi ya kampuni lazima itake into account its business interests presently and in future.

Lakini kama nilivyosema kwenye post yangu ya nyuma, this is problem rooted in our society. Kumbuka jana kulikuwa sio tuu na Miss Tanzania. Kulikuwa pia na ufunguzi wa kampeni za kisiasa huko Igunga. Kulikuwa pia na michezo ya mbalimbali. Tunachukulia issues very lightly. All go down kuwa kama serikali ingekuwa imetoa tamko tokea mapema haya yasingetokea. Hata hivyo vyombo vya habari hasa vya bara vimechangia sana haya kutokea. Nilishangaa Zanzibar disaster was trending worldwide on Twitter lakini kwenye vyombo vyetu vya habari vya ndani ilikuwa kama halikuwa janga kubwa.