Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mzee wa Miaka 84 afungua kesi ya talaka baada ya kuigiza Kiziwi na Bubu kwa Miaka 62 ili asimsikilize mkewe. mzee Barry Dawson mwenye umri wa miaka 84 kutoka Waterbury Connecticut, anaripotiwa kufungua kesi ya talaka dhidi ya mke wake, Dorothy, baada ya kuishi naye kwenye ndoa kwa miaka 62.
Sababu ya kushangaza ni kwamba mkewe aligundua kuwa kwa muda wote huo mzee huyo alikuwa akijifanya kiziwi na bubu ili kuepuka kusikiliza mazungumzo yake.
kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa, Barry aliweza kuigiza hali hiyo kwa ustadi kwa zaidi ya miaka 60 bila kuwahi kujisahau hata mara moja, hadi pale Dorothy alipogundua ukweli huo kwa bahati mbaya.
Sasa Dorothy naye anaripotiwa kuwasilisha maombi ya talaka. huku ikidaiwa kuwa hakukasirishwa sana na udanganyifu wenyewe, bali alishangazwa zaidi na jinsi mume wake alivyofanikiwa kuuficha ukweli huo kwa miaka yote hiyo.