Kampuni moja ijulikanayo kama Kingsway International au maarufu kama American Garden inaajiri wafanyakazi bila mkataba wowote, na wakati wowote inafukuza wafanyakazi bila kufuata sheria ya kazi ya nchi. Lakini vilevile inawakata mishahara kwa madai kwamba ni michango ya hifadhi ya jamii, lakini wafanyakazi hawajahi kujaza form ya mfuko wowote wa hifadhi ya jamii. Vilevile inalipa mshahara bila salary slip, mfanyakazi hajui ni kiasi gani kimepelekwa TRA kama kodi. Je, huu SI uvunjaji wa sheria za nchi? Wanajukwaa tunaomba ushauri wenu.