Taasisi nyingine pia zinavutia, ndiyo tena sana tu! Na tena zipo kada zenye mtonyo mzuri na wa maana kuliko hata huo wa TRA. Shida kubwa iko miongoni wa hawa wasomi wetu, tangu awali mtu anakuwa na wazo kuwa anataka tu kukaa kwenye kiyoyozi mda wote! Mfano, sidhani kama mpunga wa TRA unazidi ule ulioko kwenye mafuta na gesi au madini! Lakini huko hukuti utitiri kama huu!
Nadhani TRA watu wanaomba wengi kutokana na sifa za watu wanaotakiwa! Kule wanahitajika watu wamesoma uhasibu, biashara and the likes!
Kwa kawaida masomo haya yanasomwa na watu wengi sana, kuna utitiri wa vyuo kuanzia vile vya astashahada, stashahada na shahada! Kwa hiyo kunakuwa na watu wengi wenye hiyo taaluma!
Ukija uhamiaji unakuta wanachukua watu wa kada tofauti, ni lazima watu wanakuwa wengi, halafu kazi zenyewe sio za kuumiza akili, hata masomo pia sio ya kuumiza kichwa sana!