Ajira EAC ni tatizo kubwa, Watanzania 30,000 wajitokeza kufuata nafasi 400 TRA

Kweli,hapo wapo watu kibaaoooo wana kazi zao,wamependa TRA wewe.

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app
 
Ubwegenazi mkubwa sana huo, badala ya kutafuta mishe zingine unang'ang'ana na kuomba ajira za watu maelfu.

Ngw'ana Kabula
Nakumbuka yule mbunge sijui mhindi/mwarabu wa jimbo 1 kule Manyara wakati anatuomba "kazi" ya ubunge wakina chege&temba wakawa wanapiga push up pale jukwaani ye kupiga 2 akashindwa hoi kunyanyuka hawezi,ni ubwege tu kuja kutuomba ajira wananchi wkt push up hawezi.

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Kuna kazi hapa tz wakitoa nafasi utaona utitiri wa watu wakijazana kweli kweli! Nazo ni TRA, Uhamiaji, Bandari, na jeshi!

Kada nyingine huoni msururu wa namna hiyo! Mpaka sasa zinatolewa nafasi mbali mbali, lakini huko kwingine hawajai kiivyo!


Hata hivyo sikufurahia utaratibu waliotumia kwenye hili zoezi! Kwa nafasi chache kama hz, hakuna haja ya kuita watu wengi kiasi hicho! Yaani nafasi moja iwaniwe na watu kama 75 hv! hii sio fair hata kidogo!
 

Hilo bado ni tatizo, ina maana taasisi nyingine zote hazina tija hadi nyote mnataka mng'ang'anie TRA na uhamiaji. Japo ni kweli TRA huwatoa wengi, nina madogo washkaji fulani hapo makao makuu TRA wanaendesha magari mazuri. Lakini hata hivyo inafaa muhakikishe na taasisi zingine zinavutia.
 
Taasisi nyingine pia zinavutia, ndiyo tena sana tu! Na tena zipo kada zenye mtonyo mzuri na wa maana kuliko hata huo wa TRA. Shida kubwa iko miongoni wa hawa wasomi wetu, tangu awali mtu anakuwa na wazo kuwa anataka tu kukaa kwenye kiyoyozi mda wote! Mfano, sidhani kama mpunga wa TRA unazidi ule ulioko kwenye mafuta na gesi au madini! Lakini huko hukuti utitiri kama huu!
Nadhani TRA watu wanaomba wengi kutokana na sifa za watu wanaotakiwa! Kule wanahitajika watu wamesoma uhasibu, biashara and the likes!

Kwa kawaida masomo haya yanasomwa na watu wengi sana, kuna utitiri wa vyuo kuanzia vile vya astashahada, stashahada na shahada! Kwa hiyo kunakuwa na watu wengi wenye hiyo taaluma!

Ukija uhamiaji unakuta wanachukua watu wa kada tofauti, ni lazima watu wanakuwa wengi, halafu kazi zenyewe sio za kuumiza akili, hata masomo pia sio ya kuumiza kichwa sana!
 
Hakuna taifa duniani nguvu kazi yake kubwa imeajiriwa kwenye formal sector bali kwenye informal sectors.

Pamoja na kwamba sitaki kuamini hao vijana wote ni majobless lakini wabadilike mtazamo kuna pesa za bure mitaani vijana wajiunge kwenye vikundi wajiajiri kwenye kilimo na businesses nyingine nyingi.
 
Kuna watu wanakaa miaka mitano mtaani bila kazi au hata kuitwa kwenye interview.. Mimi sioni ubaya kwa UTUMISHI kuita watu wengi as long as wanavigezo as inawasaidia kuwapa watu experience.
 
Ngoja mafuta na gesi watangaze kazi uone hilo nyomi.. Ukweli ni kwamba wasomi ambao hawana kazi wamekuwa wengi mtaani thats why.. Nakuhakikishia ata wakitangaza kazi za ualimu the same nyomi litatokea
 
Ngoja mafuta na gesi watangaze kazi uone hilo nyomi.. Ukweli ni kwamba wasomi ambao hawana kazi wamekuwa wengi mtaani thats why.. Nakuhakikishia ata wakitangaza kazi za ualimu the same nyomi litatokea
Nyomi kwa walimu halijawahi kupungua, maana kila mwaka graduates ni wengi sana kwa ngazi zote!

Hoja yangu kwenye mafuta na gesi inahusu kile kinachoitwa sehemu zinazolipa, Nyomi kuwepo ni lazima maana hata huko wanasheria, wahasibu, PR ambao ni wengi mtaani wanatakiwa!
 
Ukubwa wa tatizo ni ktk kuchagua masomo ya kusoma na kuchagua kazi za kufanya .... hapo wapo waliopo ktk ajira lakini na wao waliomba hizo nafasi...

kuna fani za sheria na hizi za financial, computer huwa zina watu wengi sana... tofauti na fani kama za Physics, udaktari, Chemistry etc

na hapa ndipo tunapo kuja ona kuna tatizo kubwa sana la ajira...
 
kiukweli watanzania ni watu tusiojielewa
wakiitwa weng tunalalamika wanasumbua watu bure
wakichujwa wachache utasikia wameitana wenyewe kwa wenyewe


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…