Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Ndugu watanzania, hasa wasomi wanaograduate katika fani za Computer Science (hasa programming katika lugha mbalimbali), Engineering (hasa CAD design na analysis), English Language (hasa writing), statistics, marketing (graphic design) na Accounting. Kuna ajira nyingi sana za freelancers hutangazwa katika mitandao ya www.elance.com, www.freelancer.com, www.guru.com, www.vWorker.com na www.oDesk.com ambazo unaweza kuzifanya ukiwa hapo hapo ulipo hata kama mwajiri anaishi Marekani. Utaratibu wake ni wewe kujiandikisha kwenye mitandao hiyo (bila malipo yoyote) halafu unapitia kazi zlizotangazao pale. Iwapo utakuta kuna kazi unayoweza kuifanya, basi unatuma maombi yako kwa kushindana na wengine wanaotaka kazi ile pia (bidding.) Utaeleza ujuzi wako kulingana na kazi hiyo, na kiasi unachotaka ulipwe kwa saa au kwa kazi yote. Mwenye kazi atawasiliana nawe kwa email halafu mikubaliana mnapeana mkataba na unaanza kazi ukiwa nyumbanni kwako. Ukimaliza kazi unamtumia mwajiri huyo halafu unatumiwa pesa yako kwa njia utakayotaka mwenyewe: Paypal, Moneygram, Westernunion au hata kwa bank direct deposit ingawa hiyo huweza kuchukua muda mrefu. Kuna kazi nyingine unaweza kulipwa downpayement ya 30% to 50% kulingana na mtakavyokubaliana.
Ninavolunteer katika organization moja inayosaidia vijana kupata kazi katika mazingira ya leo ambapo kazi zimekuwa adimu, na juzi tulikuwa na kongamano fulani kuhusu kuwawezesha vijana kujiajiri na kujipata wateja wa kutoka mbali. Mtoa mada mmoja alizungumzia ajira hizo za freelancing na kuwasihi vijana wasiwe wanadai malipo makubwa sana kwa vile ni afadhali kupata kidogo kuliko kukosa kabisa. Baadaye nimekaa na kufanya utafiti wa kina kuhusu mitandao hiyo nikagundua kuwa kazi nyingi hutoka nchi za magharibi ambako labor cost ni kubwa sana, halafu watu wengi wanaozipata huwa ni watu wa Asia (hasa India, Pakistan, Bangldesh na China) ingawa siku za hivi karibuni kumekuwa na waafrika wachache kutoka Kenya na South Africa ambao wamekuwa wakizipata pia. Utakuta kazi ambayo mmarekani angetaka alipwe dola 50 kwa saa, anapatikana mtu kutoka bangladesh mwenye qualification zaidi ya yule mmarekani na yuko tayari kuifanya kazi hiyo kwa dola 5 hadi 10 kwa saa. Nina imani kuwa kuna vijana wa kitanzania wanaoweza kufanya kazi hizo pia kwa kushindana na hao wabangladesh na wakafanikiwa. Kazi nyingi zina kiwango cha masaa 40 kwa wiki, kwa hiyo mapato kati ya 200 hadi dola 400 kwa wiki ni ajira nzui sana, na hasa kumbuka kuwa unaweza kufanya kazi za namna hiyo mbili au tatu kwa mpigo na hivyo kujipatia hadi dola 1200 kwa wiki.
Haya vijana wa kitanzania, changamkieni tenda hizo!