Jpinduzi
Senior Member
- Feb 26, 2011
- 136
- 68
Ndugu Marafiki ni matumaini yangu ya kuwa tunaendelea vizuri na shughuli za kijamii pamoja na ugumu wa maisha ya kila siku.Leo hii napenda kuchangia juu ya maada ifuatayo''Ajira kwa Vijana'' hii ni changamoto iliyopo mbele yetu hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa yanayochangiwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia.Mkutano wa ''Ajira ya Vijana'' Youth Employment Summit uliofanyika Alexandria nchini Misri mwaka 2002 yalijadiliwa mambo kadhaa kubwa likiwa ni tatizo la ajira kwa vijana.
Sera ya ajira,ajira ya vijana ipo katika maeneo mawili sekta rasmi (Formal sector) na sekta isiyo rasmi (Informal sector).Katika sekta rasmi vijana utegemea kuajiriwa na kulipwa mishahara,sera ambayo kwa hapa Tanzania na kwingineko duniani serikali zimekwisha jitoa.Hapa Tanzania hali hii imesababisha uchumi kuporomoka na hivyo hivyo ukosefu wa ajira kuongezeka kwa kuwa maeneo ya ajira kama viwanda,mashirika,mashamba makubwa yamebinafsishwa baada ya kuhindwa kujiendesha kwa faida.
Baada ya ubinafsishaji viwanda,mashirika n.k vimekuwa katika hali ya kuleta mabadiliko yenye ushindani lakini kwa kiwango cha chini bila mafanikio makubwa.Pia tatizo lingine ambalo naliona ni ukosefu wa mfumo mzuri wa elimu kwa vijana,hali hii inasababisha vijana wengi kushindwa kupata ajira pindi wamalizapo shule kutokana na kukosa elimu ya vitendo,mashuleni ufundishwa zaidi nadharia ambayo haiendani na mazingira halisi.
Pia kwa mawazo yangu nafikiri kuwa serikali lazima ifanyie mabadiliko sera ya uwekezaji.,wawekezaji watoe kipaumbele na kuongeza ajira kwa vijana wenye sifa ikiwa ni pamoja na kuwaendeleza kitaaluma ili waweze kutoa mchango mkubwa kwa taifa lao ambalo linawategemea kwani wao ndio nguvu kazi.Pia serikali isiruhusu uwekezaji holela kama kuwekeza katika kutengeneza dawa za kienyeji,ukulima wa matunda na nyingine nyingi shughuli hizi waachiwe vijana na wazawa.Vijana waelimishwe juu ya mambo yanayowahusu kama vile kujua sera za maendeleo zinazowahusu wao.
mimi naamini vijana wakiwezeshwa wanaweza endapo watajituma na kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa yao na wengine.Ahsanteni​