SoC04 Ajira kwa watumishi tarajali (internship)

SoC04 Ajira kwa watumishi tarajali (internship)

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
May 23, 2013
Posts
7
Reaction score
14
Tarajali ni kipindi ambapo wafanyakazi hupokea mafunzo ya kazi chini ya uangalizi maalumu katika shirika ama kampuni fulani kwa kipindi cha muda fulani ili kupata uzoefu utakao muongezea thamani katika kazi yake ili apate soko katika ajira kirahisi.

Hapa tanzania tuna taasisi inayowasaidia vijana kupata mafunzo tarajali inayoitwa TaESA(Tanzania Employment Services Agency). Imesaidia vijana wengi kupata nafasi za ajira ya kudumu na za muda mfupi pia.

Ni taasisi inayotoa nafasi za ajira za kudumu kwa taasisi binafsi tu ila sio kwa taasisi za kiserikali kwa sababu serikali inatumia mfumo mmoja tu wa ajira ambao unapitia taasisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora .

Hii inasababisha vijana wengi wasipate nafasi za ajira kiurahisi kwa sababu wana nyanja chache, ni labda wakatafute ajira kwenye taasisi binafsi au wapambane na utumishi ilihali kuna vijana ambao tayari wameshapokea mafunzo tarajali yaliyowafanya wawe wafanyakazi wazuri katika kile wanafanya.

Taasisi nyingi za kiserikali imekua ikichukua fursa ya kuwatumia vijana wabobevu waliopokea mafunzo tarajali kuwafanyisha kazi pasipo na stahiki nzuri, na kwa sababu ajira imekua changamoto wamejikuta wakitumikia miaka mingi pasipo na tumaini au stahiki nzuri zitakazoendesha maisha yao vizuri.

Nilikua napendekeza serikali itoe nyanja zingine za ajira kuliko kutegemea utumishi peke yake ili kutoa options nyingi za ajira ukizingatia hata TaESA pia ni taasisi ya kiserikali na pia watu wanafanya interview wakipokelewa TaESA na hata taasisi zinazowapokea pia, hivyo unakuta mtu anapigishwa interview hata mara mbili.

Tukisema vijana wategemee tu utumishi kwa ajili ya ajira tutakua tunarudi nyuma sana, kuna taasisi zilizopo ulaya zinaanza kuhusisha ujuzi wa mtu katika ajira na sio tu elimu yake ya chuo, na hii inpelekea kupata vipaji ambavyo huenda havikupitia chuoni ila walijifunza wao binafsi, hawa nao wangehusika katika kuajiriwa pia.

Hii ni kwa sababu ya ukuaji wa teknolojia ambako vijana wengi hujifunza vitu vingi kupitia huko na kama serikali inapaswa kutafuta namna itakavyowahusisha vijana hao katika ajira.

TaESA isiwe taasisi ya kupata vibarua (cheap labor) bali iwe sehemu moja wapo ya vijana kupata ajira ya kudumu kama watoayo utumishi.
 
Upvote 5
Back
Top Bottom