KERO Ajira mpya Halmashauri ya Wilaya Kilindi hatujalipwa pesa za kujikimu

KERO Ajira mpya Halmashauri ya Wilaya Kilindi hatujalipwa pesa za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

klev

New Member
Joined
Sep 14, 2026
Posts
1
Reaction score
0
Baada ya kuajiriwa, hatukulipwa fedha za kujikimu kama inavyopaswa. Tuliingizwa kwenye mfumo wa malipo (payroll) na kuanza kuripoti kazini, lakini stahiki hizo bado hatujazipokea.

Kutolipwa fedha za kujikimu kumesababisha changamoto kubwa katika maisha ya kila siku, kwani baadhi yetu tunalazimika kuishi katika mazingira magumu wakati tukitekeleza majukumu yetu ya kazi.

Tunaiomba mamlaka husika kufuatilia suala hili na kuhakikisha fedha hizo zinalipwa kwa wahusika kwa wakati.
 
Back
Top Bottom