Ajira Mpya Halmashauri Ya Wilaya Ya Mafia 2025/2026 – Stahiki za kujikimu hazijalipwa

Ajira Mpya Halmashauri Ya Wilaya Ya Mafia 2025/2026 – Stahiki za kujikimu hazijalipwa

Mdeke_Pileme

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2013
Posts
1,599
Reaction score
2,248
Ninaandika hapa kuwasilisha kero inayotukumba sisi baadhi ya watumishi wapya wa Afya wa Halmashauri ya Mafia tulioajiriwa mwaka 2025/2026.

Mpaka sasa, watumishi hatujalipwa hatujalipwa kabisa hela ya kujikimu, bila maelezo yoyote rasmi kutoka kwa wahusika. Hali hii inaleta maswali makubwa juu ya:
  • Uadilifu katika mchakato wa malipo
  • Usawa kwa watumishi walioajiriwa kwa wakati mmoja
  • Ufanisi wa mifumo ya kiutawala
Tumefika kazini, tunatekeleza majukumu yetu kikamilifu, lakini haki yetu ya msingi bado haijatimizwa.

Tunaiomba Halmashauri Ya Mafia:
  • Kutoa ufafanuzi rasmi kuhusu ucheleweshaji huu
  • Kuhakikisha watumishi wote wanalipwa stahiki zao bila ubaguzi
  • Kurekebisha hitilafu yoyote ya kiutawala iliyopo

Tunaamini haki na usawa vinapaswa kuzingatiwa kwa kila mtumishi.

#HakiKwaWatumishi
#AjiraMpya
 
Back
Top Bottom