Ninaandika hapa kuwasilisha kero inayotukumba sisi baadhi ya watumishi wapya wa Afya wa Halmashauri ya Mafia tulioajiriwa mwaka 2025/2026.
Mpaka sasa, watumishi hatujalipwa hatujalipwa kabisa hela ya kujikimu, bila maelezo yoyote rasmi kutoka kwa wahusika. Hali hii inaleta maswali makubwa juu ya:
Uadilifu katika mchakato wa malipo
Usawa kwa watumishi walioajiriwa kwa wakati mmoja
Ufanisi wa mifumo ya kiutawala
Tumefika kazini, tunatekeleza majukumu yetu kikamilifu, lakini haki yetu ya msingi bado haijatimizwa.
Tunaiomba Halmashauri Ya Mafia:
Kutoa ufafanuzi rasmi kuhusu ucheleweshaji huu
Kuhakikisha watumishi wote wanalipwa stahiki zao bila ubaguzi
Kurekebisha hitilafu yoyote ya kiutawala iliyopo
Tunaamini haki na usawa vinapaswa kuzingatiwa kwa kila mtumishi.