RESOLVED KERO Ajira Mpya (Kada ya Afya) Singida Mjini na Mkalama tumepewa nusu Fedha ya Kujikimu, wanasema Serikali haina fedha

RESOLVED KERO Ajira Mpya (Kada ya Afya) Singida Mjini na Mkalama tumepewa nusu Fedha ya Kujikimu, wanasema Serikali haina fedha

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ajira mpya wa sekta ya afya—tulioripoti kazini Januari 2026 katika Manispaa ya Singida Mjini na Wilaya ya Mkalama.

Mimi ni Tabibu Msaidizi Daraja la Kwanza. Tulitarajia kulipwa fedha za kujikimu kiasi cha shilingi milioni moja na laki mbili (1,200,000), lakini tulicholipwa ni shilingi laki sita (600,000) tu. Malipo haya tuliyapokea Jumamosi, tarehe 16, bila maelezo ya kuridhisha kuhusu punguzo hilo.

Tukiuliza tunaambiwa serikali haina fedha, lakini cha kushangaza baadhi ya wenzetu wamelipwa kiwango kamili. Hali hii inaleta sintofahamu kubwa na hisia za kutokuwa na haki.

Kinachotusikitisha zaidi ni kwamba tunapohoji, tunaambiwa tukope kwanza ili kujikimu—tena kutoka kwa wakopeshaji wa mtaani wenye riba kubwa hadi asilimia 25. Ushauri huu unatolewa na mtumishi wa manispaa, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.

Soma Pia: Chamwino Kada ya Afya tulioripoti March 2025 hatujalipwa fedha za kujikimu, Viongozi wanatupuuza

Tunaomba mamlaka husika, ikiwemo Wizara ya Afya, itusaidie kufuatilia suala hili. Je, viongozi wanahusika wanalifahamu tatizo hili? Kwa nini kuna tofauti ya malipo kati ya watumishi wenye hadhi moja?

Tunaomba tupatiwe haki yetu ya malipo kamili ya fedha za kujikimu, kwani hali hii inatunyima utulivu na kuathiri maisha yetu kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom