A
Anonymous
Guest
Habari za majukumu, JF.
Sisi watumishi wa ajira mpya wa Januari 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba (Momba DC) bado hatujapokea fedha zetu za kujikimu hadi leo, wakati watumishi wa halmashauri nyingine tayari wamelipwa.
Jambo linalotusikitisha zaidi ni kwamba tunapofuatilia stahiki zetu hatupewi majibu ya kueleweka. Badala yake, baadhi yetu tunapewa vitisho kwamba tunafuatiliwa kwa kudai haki zetu. Kila mara tunaambiwa malipo yako "kwenye mchakato", ilhali tunaelezwa kuwa fedha tayari zimeshatolewa kutoka Hazina na kinachosubiriwa ni kukamilishwa kwa taratibu za halmashauri.
Tunaomba mtusaidie kupaza sauti yetu ili mamlaka husika zitoe ufafanuzi na kutekeleza malipo haya haraka. Hatuoni sababu ya Halmashauri ya Momba kuendelea kuchelewa wakati halmashauri nyingine tayari zimewalipa watumishi wao. Tunachoomba ni haki yetu.