EzekielEmanuel1997
New Member
- Jul 29, 2022
- 4
- 11
1.0 Ikisiri
1.2 Utangulizi
2.0 Nini Kifanyike
2.1 Ajira zote Mpya Serikalini Ziwe za Awamu (Miaka Kumikumi)
3.0 Hitimisho
Mbali na maoni haya, serikali pamoja na wadau inatupasa kuupitia upya mfumo wetu wa elimu kwani huo ndiyo chanzo cha changamoto hii. Hatuna budi kujisahihisha mapema kwani hakuna changamoto isiyo na madhara hasi.
[1] Msemo Keki ya nchi una maana “Mshahara”
Nchi nyingi duniani zinakumbana na changamoto ya ajira kwa vijana. Hii ni kutokana na ongezeko la idadi ya wahitimu katika ngazi mbalimbali za elimu ingali hapajatengenezwa mazingira rafiki kwa ajili ya kuwaajiri au kujiajiri vijana hao. Pamoja na kuonekana madhara makubwa ulimwenguni kote, nchi za Afrika na Asia zimeonekana kukumbwa zaidi na madhara haya ikilinganishwa na nchi za Ulaya. Hivyo mjadala wa makala hii umekitwa zaidi katika nchi za Afrika na Asia, Tanzania ikichukuliwa kama sampuli kifani. Kwa hiyo, katika makala hii, mwandishi analenga kutoa maoni kuhusiana na namna ya kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana kwa kuzingatia kwamba nchini Tanzania kama ilivyo kwa nchi zingine tatizo hili linazidi kukua na matokeo yake yanatarajiwa kuwa ni mabaya.
1.2 Utangulizi
Mjadala wa makala hii unazingatia ukweli kwamba, elimu rasmi kwa nchi za Afrika na Asia ni matokeo ya mfumo wa elimu ya kikoloni. Itakumbukwa kwamba adhma ya elimu ya kikoloni ilikuwa ni kuandaa watendaji ambao wangerahisisha ufanyaji wa kazi za uzalishaji mali, shughuli za kiutawala pamoja na kuandaa vibaraka wa kisiasa. Elimu hii haikuwa na lengo la kumuandaa Mwafrika katika kujitegemea kiutawala, kifikra n.k. Hivyo, asilimia kubwa ya wahitimu waliona kuajiriwa ndiyo matokeo ya kupata elimu. Mawazo na tajriba zao zikawa katika mwegamo huo. Kwa hiyo, miongo na miongo mfumo huo ukaendelea mpaka miaka ya leo. Baada ya nchi za nyingi hususani za Afrika kupata uhuru, ziliendeleza mfumo uleule wa elimu huku zikijaribu angalau kuubadili mfumo wa elimu ya kikoloni ingawaje hazikufanikiwa kama ilivyotarajiwa. Mfano mzuri ni Elimu ya Ujamaa na Kujitegemea iliyoanzishwa na Mwl. J.K. Nyerere. Mfumo huu haukufanikiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo shinikizo kutoka nchi za Magharibi. Hivyo, kwa asilimia kubwa bado tunaogelea katika dimbwi la elimu ya mkoloni ambayo inamuandaa kijana kuajiriwa na si kufikiri katika kutengeneza namna ya kujiajiri. Kwa kuzingatia usuli huu, makala hii inalenga sasa kutoa maoni ya namna ya kukabiliana na hii changamoto.
2.0 Nini Kifanyike
Waandishi wengi wameandika kuwataka vijana wajiajiri na mapendekezo mengine. Sitarudia kilichosemwa na waandishi bali ninatofautiana nao kidogo kimtazamo kwa kuwa vijana wengi wanajitahidi kujiajiri lakini bado matarajio hayafikiwi na kila siku idadi ya watu wasio na ajira inaongezeka. Mwandishi wa makala hii anaona jambo linalofaa ni:
2.1 Ajira zote Mpya Serikalini Ziwe za Awamu (Miaka Kumikumi)
Kutokana na sheria za Tanzania, asilimia kubwa ya waajiriwa serikalini wanapaswa kustaafu katika umri miaka 60. Yaani, iwapo mwajiriwa ataajiriwa akiwa na miaka 30 basi ana miaka 30 ya kula keki ya nchi[1] kisha kupatiwa mafao. Hii ni sawa na kusema kwamba, sheria inaruhusu katika miaka yote hii 30 nafasi hii kumilikiwa na mtu mmoja mpaka pale atakapohamishwa kituo, kufa au kufukuzwa kazi. Ni sawa na kusema vilevile kwamba, katika miaka hii 30 kama yupo mwenye sifa ya kuajiriwa atapaswa asubiri mpaka pale mtangulizi wake atakapofikia umri wa miaka 60, atakapokufa au kuhamishwa/ kufukuzwa kazi. Madhara ya sheria hii ni haya yafuatayo.
Kwanza, idadi kubwa ya watu wasio na ajira ilhali wana sifa za kuajiriwa inaongezeka kwa kasi. Hii inachagizwa vilevile na kutokuwapo kwa mikakati ya kuongeza nafasi za ajira ilhali idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu inaongezeka kwa kiwango kikubwa kila mwaka. Tafiti za hivi karibuni zinaonesha jumla ya wahitimu zaidi ya laki moja huhitimu kila mwaka.
Pili, waajiriwa wengi wamekuwa wakiridhika na ajira wasiwaze namna ya kuongeza mapato yao nje na ajira. Kutokana na saikolojia kuwafariji waajiriwa serikalini kwamba wana muda mrefu katika ajira, kumefanya waajiriwa wengi waendelee kula keki ya nchi wasijihusishe na shughuli mbalimbali mathalani kilimo bora, ufugaji, biashara n.k ambazo zingekuwa na tija katika maisha yao nje na ajira. Jambo ambalo lingeweza kupunguza ukali wa maisha yao pamoja na wale wasio na ajira
Tatu, hali ya uchumi wa kudumaa. Neema ya kuwapo kwenye ajira mpaka ufikiapo miaka 60 inachangia kwa kiasi kikubwa kufanya uchumi wetu kudumaa. Hii ni kutokana na sababu kwamba mzunguko wa fedha haupo katika uzalishaji bali upo katika matumizi. Hakuna hofu ya mtetereko wa kiuchumi ambayo inawazwa na waajiriwa wengi. Wengi wanafanya matumizi yaliyo nje na bajeti wakijua kwamba mwisho wa mwezi kuna keki ya taifa. Ni rahiri vilevile kujiingiza katika madeni yasiyo na tija kutokana na tu na kuwapo kwa keki itakayotumika kulipa hayo madeni. Hali hii inadhorotesha uchumi wa nchi kwani matokeo ya mwisho kabisa yanamgusa yule asiye na ajira kutokana na mzunguko wa fedha kuwa mgumu kwake ilhali mwepesi kwa wenye keki ya taifa.
Hivyo, kutokana na hali hiyo iko haja ya kuangalia na kuafiki kupunguza miaka ya ajira na kuzifanya ziwe ni za awamu kila baada ya miaka kumi. Yaani iwapo mtu ataajiriwa leo, basi atambue kwamba ana miaka kumi ya kula keki ya taifa kisha ataachia nafasi hiyo kwa mtu mwingine ambaye naye atafanya kwa miaka kumi kisha awamu ya pili inamalizika kwa yule wa kwanza. Kwa hiyo, mwajiriwa serikalini atakuwa na jumla ya miaka 20 pekee ya kula keki ya taifa.
Hii itasaidia mwajiriwa kujiandaa kisaikolojia kwamba anao muda mchache wa kula keki ya nchi. Hivyo, kupitia mshahara wake atafikiri namna ya kujiongezea kipato kabla na baada ya ajira. Mzunguko wa fedha kitaifa utakua hatimaye kupoza makali ya ugumu wa maisha kwa watu wote kwa sababu uzalishaji mali utaongezeka. Kikubwa zaidi, ni kwamba tatizo la ongezeko la vijana wasio na ajira litapunguzwa mara mbili ya hali iliyopo sasa kwani kila baada ya miaka kumi walioko kwenye ajira watapisha wengine. Vivyo hivyo kwa awamu itakayofuata. Mbali na hayo yote mfumo wa namna hii utasaidia kuondoa sononeko la kisaikolojia miongoni mwa wahitimu wa vyuo kwani kwa kufanya hivi kutaleta angalau hali ya usawa katika kula keki ya nchi. Vilevile, bidii ya kujituma ns kuzalisha mali itaongezeka miongoni mwa waajiriwa kutokana na muda mchache walionao katika kuzitumia rasilimali fedha watakazokuwa wakilipwa serikalini.

Upvote
30