Zilipotoka ajira za walimu wapya, tayari serikali ilishapiga hesabu na kutoa fungu ambalo lilipelekwa moja kwa moja eneo husika wilaya au mkoa.
Baadaye vijana wetu wameitwa kwenye mkoa husika ili wapeleke makaratasi yenye taarifa zao kwa ajili ya uhakiki.
Makosa au tuseme uhuni umeanza hapa, kwamba baada ya kufikisha taarifa zao, wamepewa likizo, ikiwa ni kwamba wameunganishwa na walimu waliopo likizo hivyo shule zitakapogungiliwa wanarudi na kupangiwa vituo vya kazi.
Mkasa ni hapa, shule zimefungiliwa vijana wanapigiwa simu wasiende sababu taarifa zao...