Mh. Rais Angalia Unaharibiwa na Mkurugenzi wa Wilaya, Mkoa, Hii Mbaya Sana.

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,266
Reaction score
25,555
Moja kwa moja kwenye mada.

Zilipotoka ajira za walimu wapya, tayari serikali ilishapiga hesabu na kutoa fungu ambalo lilipelekwa moja kwa moja eneo husika wilaya au mkoa.

Baadaye vijana wetu wameitwa kwenye mkoa husika ili wapeleke makaratasi yenye taarifa zao kwa ajili ya uhakiki.

Makosa au tuseme uhuni umeanza hapa, kwamba baada ya kufikisha taarifa zao, wamepewa likizo, ikiwa ni kwamba wameunganishwa na walimu waliopo likizo hivyo shule zitakapogungiliwa wanarudi na kupangiwa vituo vya kazi.

Mkasa ni hapa, shule zimefungiliwa vijana wanapigiwa simu wasiende sababu taarifa zao zimechelewa kufika.

Kisa hiki hapa, wenzao walioitwa pamoja mkoa jirani wametumiwa fungu lao, muda huu wapo kazini.

Wanawapigia simu, wasije hadi mwezi wa nane wkt mshahara wa mwezi huo utakapotoka.

Nilichogundua baada ya kuambiwa ni kuwa kuna mchezo mchafu wa mkurugenzi na wasaidizi wake wanatakatisha pesa ya jasho la watu wengine.

Nipo Nzega kwa sasa na hivi Jumatatu naingia hapo ofisini kwa Mkurugenzi nijue kama na yeye anafanya huo mchezo mchafu.

Na je walimu wote waliopangiwa kazi kwa mkoa au wilaya yake wamesharipoti kwenye vituo vyao?.

Mheshimiwa Rais, hawa hawa wakurugenzi unaowategemea kwenye uchaguzi ndiyo hawa hawa wanakuharibia huku chini.

Na walimu hawa hawa ndiyo unawategemea kukupigia kura ndiyo hawa mkurugenzi anacheza nao mchezo wa paka na panya.

Nawasilisha kutoka Nzega.
 
Pambaneni na hali yenu pamoja na sa100 wenu

#NRNE
 
Wewe hutafaa kuwa mtumishi wa umma sijui umepataje ajira
 
Pambaneni na hali yenu pamoja na sa100 wenu

#NRNE
Sawasawa, katika hawa ninao wapambanania naona kabisa mmoja wa ndugu yako usiye kuwa na taarifa zake yupo humo naye anapitia madhira haya!.

NRNE.
 
Back
Top Bottom