ram
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 9,326
- 8,505
Tangu ajira za walimu zimetangazwa nimekuwa nikiona humu jamvini watu wakitaka kujua jinsi maeneo yalivyo huko walikopangiwa, mimi ofisi zangu ziko attached kwenye halmashauri ya Musoma Vijiji, kwakweli sijaamini, mwitikio ni mkubwa, walimu wamekuja kwa wingi na hivi wako hapo nje na masanduku, magodoro wanasubiri kusafirishwa kupelekwa kwenye vituo vyao vipya vya kazi. Hongereni walimu mliopangiwa mkoa wa Mara hususani halmashauri ya Musoma vijijini, manake sikuona hata mtu mmoja anauliza vipi kuh mkoa wa Mara.