Ajira mpya za walimu, mwitikio ni mkubwa

Ajira mpya za walimu, mwitikio ni mkubwa

ram

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
9,326
Reaction score
8,505
Tangu ajira za walimu zimetangazwa nimekuwa nikiona humu jamvini watu wakitaka kujua jinsi maeneo yalivyo huko walikopangiwa, mimi ofisi zangu ziko attached kwenye halmashauri ya Musoma Vijiji, kwakweli sijaamini, mwitikio ni mkubwa, walimu wamekuja kwa wingi na hivi wako hapo nje na masanduku, magodoro wanasubiri kusafirishwa kupelekwa kwenye vituo vyao vipya vya kazi. Hongereni walimu mliopangiwa mkoa wa Mara hususani halmashauri ya Musoma vijijini, manake sikuona hata mtu mmoja anauliza vipi kuh mkoa wa Mara.
 
watu wamesota mtaani for long...sasa hivi ukipangwa kokote lazima uende...waombe wasitoroke ndugu yamgu
 
Wanakuja kula hela za kujikimu wakimbie hao
 
kwa mwl amayejua kazi yake hii ni nafasi pekee ya kujiendeleza kielimu then kufikia malengo mtaan bila kazi noma
 
...Natumai Serikali hii iliyozidiwa na ukata haitawakopa mishahara na marupurupu yao mengine ya kusafiri na toka eneo moja hadi jingine pamoja na gharama za kusafirisha mizigo yao.
 
...Natumai Serikali hii iliyozidiwa na ukata haitawakopa mishahara na marupurupu yao mengine ya kusafiri na toka eneo moja hadi jingine pamoja na gharama za kusafirisha mizigo yao.[/QUmh lets pray iwe hivyo
 
Hela za kujikimu walipewa, wasiwasi wangu ni mashahara
 
Kuna jamaa yangu kashalamba hela ya kujikimu na kaingia mitini hategemei kurudi tena! Sijui watampataje!
 
sio wote waliopewa....kuna wengine wanazinguliwa but i think ni uzembe wa watu wachache....ishu kubwa je watakapopewa hizo hela watabaki kufanya kazi???
Tuombe Mungu wawe na moyo wakubaki tulikomboe taifa kwa elimu
 
Back
Top Bottom