SoC02 Ajira na vijana baada ya elimu

SoC02 Ajira na vijana baada ya elimu

Stories of Change - 2022 Competition

JOHNJOH

New Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
4
Reaction score
2
AJIRA NA VIJANA BAADA YA ELIMU

Vijana ni kundi linalochangia maendeleo ya uchumi katikataifa. Yapo makundi mbalimbali ya vijana katika taifa letu ilanitayagawanya katika makundi matatu. Kundi la kwanza kuanzia miaka 18 hadi 25 kundi hili linapatikana katikaNyanja mbalimbali za elimu kwa mfano kuanzia kidato cha kwanza hadi vyuo vikuu.kundi la pili nikuanzia miaka 26 hadi 30. Kundi hili ni la vijana walio hitimu elimu katika Nyanja mbalimbali na kundi la mwisho ni kundi kuanzia miaka 30 nakuendelea hawa ni wajiriwa na walio jiajiri wenyewe katikanyanjaa mbalimbali za kiuchumi. Vijana wengi wamekuwawakitegemea ajira za kuajiriwa baada ya kuhitimu masomo yao. Hili limekuwa tatizo kubwa katika taifa kwani vijanawengi wamekuwa hawajishughulishi na kufikiria nje ya box wamekuwa wakifikiria katika kuajiriwa tu.

Vijana wengi baada ya kuhitimu elimu ya vyuo vikuuwamekuwa wakilalama na kulalamika kutokana na uhaba waajira. Wengi wao wamekuwa wakiwategemea wazazi waokatika maswala mazima ya fedha, kula, mavazi pamoja nawaswala mazima ya vocha.Kwa kweli inasikitisha kuonakijana kutegemea ela ya vocha kwa wazazi wake.Wakatiumefika kwa vijana kujishughulisha na kuwaza nje ya box pindi wanapo kuwa masomo.

NI KWELI WAHENGA WANASEMA MSHIKA MAWILI MOJA HUMPONYOKA ila kwa nyakati hizi za utandawazi lazima mwanafunzi awe somani na kupewa elimu ya kujiajiri kwa maendeleo ya jamiina taifa nzima. Elimu ya kuajiri ni bora na muhimu sana kwavijana wa vyuo vikuu na vyuo vya kati hii itawasaidia kwaasilimia kubwa kujiajiri kwa maendeleo mapana yataifa.Taasisi mbalimbali na jumiya mbalimbali zinapaswakutoa elimu kwa vijana mbali na taasisi hizo pia wadau waelimu wanayo nafasi kwa vijana na ajira kwa uchumi wataifa.Kipi kifanyi ili kuwasaidia vijana kujiajiri na kutoamawazo ya kuajiriwa.

Nini kifanyike ili kijana aweze kujiajiri katika jamii inayomzunguka?
Elimu ya ujasiriamali kwa vijana; Elimu ni swala la msingi katika Maisha ya mwanadamu, elimu humpa mtumwanga, njia, maarifa na uelewa wa kutatua mataitizo mbalimbali katika jamii. Ni elimu ipi itakayo msaidia mwanfunzi wa chou kikuu na vyuo vya kati? Elimu yaujasiriamali ni elimu muhimu na kwa asilimia kubwa inawezakumkomboa mwanafunzi yeyote katika ngazi yoyote ya elimu.

Kupitia elimu ya ujasiriamali itamsaidia kijana kujiajirina kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa taifa. Ushauriwangu kwa wadau na serikali kwa ujumla ni kuwa navipindi, muda maalumu kwa wanafunzi au vijana kujifunzaujasiriamali tena kwa vitendo.Na mitihani iwe kwa kila kijanakuwa na kazi ya ujasiriamali tena kwa vitendo. Hii itawasaidiavijana kufikiria nje ya box na kujishughulisha. Pia itawasaidiakupunguza vijana wategemezi na kutengeneza vijanawabunifu katika sekta ya uchumi.

Mikopo yenye riba nafuu kwa vijana; Mikopo na riba nafuuni swala muhimu kwa vijana wenye nia ya kuanzisha biasharazao. Asilimia kubwa ya vijana wametoke katika familiaduni/maskini. Hivyo swala la mitaji kwao ni changamoto kwaasilimia kubwa. Wadau mbalimbli na serikali kwa ujumlawanapaswa kutoa mikopo kwa vijna na hiyo mikopo iwe yariba nafuu. Vijana wengi huwa na nia kubwa ya kujiajiri ilachangamoto ni mitaji. Mashirika ya kibenki na taasisimbalimbali zinapaswa kuwasaidia vijana katika maswala yamikopo. Kupitia mikopo itakayo tolewa itawasaidia vijanawengi kuto kata tamaa katika kujishughulisha na kuanzishabiashara zao. Sio tyu biashara pia vijaan wana uwezowakuanzisha viwanda vidogo na vikubwa katika taifa; letuishu kubwa ni mitaji ila pakiwepo na uwezekano wa kuwa namikopo vijana wengi watapata nafasi ya kuanzisha viwandavikubwa na vidogo kwa ujumla.hivyo basi mikopo ni muhimusana kwa vijana kujiajiri.

Makongamano ya vijana na kuwakutanisha vijana na watu waliofanikiwa katika Maisha; Matifa yaliyo endeleahuwa yanawakutanusha vijana na watu walio fanikiwa katikaMaisha.Kwa mfano nchi ya china huwa inaandamakongamano na watu mashuhuru walio fanikiwa katikaNyanja mbalimbli za Maisha. Kwa mafano JACKMA ni Tajiri mkubwa wa china na dunia kwa ujumla na ni mwanzilishi wakampuni ya ALIBABA.

Kila baada ya mwezi huwa anakutanana vijana kuwaelezea siri ya mafanikio yake na kuwashaurivijana wasikate tamaa. Sio tu katika taifa la china pia katikataifa la Marekani. Wapo matajiri wakubwa na wafanyabiashara wakubwa ambao hukutana na vijana nakupeanamawazo kuhusu maswala ya biashara na uwekezaji. Wafanyabiashara hukutana na vijana kila baada ya miezi kazaa naakuwapa vijana mbinu na njia za kufanya biashara. Kupitihaya makongamano yatamsaidia kijana kutoogopa kuanzishabiashara.Pia kijana atapata mbinu mbambali za kuanzisha nakufanya biashara.

Serikali kutoa support kwa vijana; Serikali inamchangomkubwa kwa vijana. Serikali inapaswa kutoa mchango nakuwasaport vijana wenye nia ya kuanzisha kampuni au biashara zao. Vijana wengi wanahitaji mitaji, ushauri, pamojana masoko.

Hii itawasaidia vijan wengi kutokuwa na hofu yakuanzisha au kujiingiza katika ujasirimali.vijana wengiwanahitaji mchango mkubwa kutoka kwa serikali. Pia serikaliinapaswa kutoa support kwa vijana wenye vipaji kwani vipajiniuppeke alionao mtu katika kufanya jambo Fulani.

Tanzaniaina vijana wengi wenye vipaji kwa mfano wapo vijana waliofanikiwa kutengeneza magari, silaha, umeme, mashine, vituo vya redio na n.k. Pia wapo vijana walio jiingiza katika kilimonao wanahitaji support kutoka kwa serikali.

Mitaji kwa vijana; Changamoto kubwa ya vijana nimitji. Vijana wengi wamekuwa wakijitahidi kuanzishabiashara mbalimbali na kampuni mbalimbali. Ila tatizo kubwani mitaji. Hivyo basi serikali inapaswa kutenga bajeti kwa ajiliya vijana wanaopenda kujiajiri katika Nyanja mbalimbali za uchumi kama vile biashara, kilimo, ujasiriamali, elimu, nautandawazi. Vijana wengi wanayondoto za kuwa matajiri nakuwa na biashara kubwa ila changamoto ni mitajai.

Garama za kusajili kampuni au biashara kuwakubwa;Kwa kweli vijana wengi wanapo asisha biashara zaonje ya mitaji kuwa changamoto pia swala usajili wa biasharaau kampuni zipo juu sana hivyo vijana wengi wanashidwakustahimili au kushidwa kusajili biashara zao.Hii imepelekeavijana wengi kukata tamaa na kuwa na hofu ya kuanzishabiashara zao hivyo kuwafanya vijana kurudi nyumbani nakuwategemea wazazi..serikali ingejaribu kupunguza garamaza usajili wa biashara.

Kodi; Maendeleo huletwa na wananchi pamoja na serikali husika kusimamia vizuri kodi za wananchi katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi. Kwa mfanobarabara, elimu, afya, viwanda, n.k. Vijana wengi wanapojiingiza katika biashara hukutana na kodi nyingi. Vijana wengi hukatatamaa pindi wanaposhridwa kuzilipa. vyema vijana kupewamuda wa kulipa kodi kwani anapojiingiza katika biashara kwamfano kupewa mwezi mmoja mara baada ya kuanzishabiashara ili kumpunguzia kijana mzigo.

Hitimisho; Vijana wana mchango mkubwa katika jamii pale watakapo wezeshwa. Vijana wanapenda kujiajiri. Changamotoni aina ya elimu inayotolewa. Pia mazingira wanayokulia(soma uje uajiriwe maneno kutoka kwa wazaziwoa)Pia changamoto ya mitaji ni sababu ya vijanakutojiajiri. Serikali na wadau kuwasaidia vijana katikakujiajiri. HII ITAWASAIDIA KWA KIASI KIKUBWA VIJANA KUJIAJIR.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom