Nina ofisi ya kisasa ya ushonaji iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam, na kwa sasa ninatafuta fundi mtaalamu mwenye uzoefu na uwezo wa kushona suti za kiume katika viwango vya juu vya ubora (Premium & Bespoke Tailoring).
Ninahitaji fundi mwenye uelewa wa kitaalamu wa suit construction, kuanzia pattern drafting, precision cutting, fitting, assembly hadi final finishing. Awe na uwezo wa kutengeneza suti zenye muonekano wa kisasa, zinazokaa vizuri mwilini (excellent fit), zenye ushonaji safi, umakini wa hali ya juu na finishing inayokidhi matarajio ya wateja wanaothamini ubora.