Namuchi braver
Member
- Nov 16, 2020
- 54
- 84
Kwa masikitiko makubwa kwa vijana wanaosoma na wazazi kusomesha.
Jana nimeshuhudia wimbi kubwa la Majobless wa Leo na baadae. Ni baada ya kuhudhuria usaili wa kazi za kukusanya taarifa za makazi na postikodi.
Nafasi zilikuwa 415 tu kwa Manispaa ya Morogoro ila idadi ya waombaji ni 5500 hivi.
Sasa kwa uwiano wa waombaji na nafasi hata nusu haijafika, ni hatari mno.
Ushauri kwa vijana Wenzangu. Ni vyema kuondoa mawazo ya kuajiliwa na kupandikiza mawazo ya kujiajiri kwani kwa kutegemea ajira na hali iliyokuwepo unaweza ukakata tamaa ya maisha.
Kwenye elimu, Wazazi ni vyema ukamwambia mwanao mapema juu ya hatari ya kusoma elimu isiyo kuwa na ufundi ndani yake mfano ualimu na kazi nyingine.
Pia ni vizuri kuhamasisha watoto wetu kupenda shughuli halisi za jamii zetu kama kilimo na ufundi licha ya ukweli kwamba huko nako kunachangamoto lakini hutashindwa kuishi kupitia shughuli hizo. Ni Morogoro Manispaa me nimekosa kabisa imani ya kupata kazi yenyewe๐๐๐