Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 43,960
- 77,533
Kutoenda kwenye usaili kwa hiyari ni sawa lakini siyo sahihi sana.Haina tofauti na kuzira kupiga kura ya kuchagua viongozi kwa sababu hukupendezwa na yaliyopita.Au,kugoma kuishi katika ndoa(kuwa katika mahusiano ya mahaba)kwa sababu tu kuna mtu alikuudhi siku zilizopita.Yote hayo ni kujipoka haki halali uliyoishika mkononi.Sawa mkuu.. Lakin duuh kama hali ndo ilivyo nikisikia hata sitaenda tena
Nipo katika kundi hili mimi😭😭Mwezi wa 6 kontena lingine la graduates linaingia mtaani likiwa na kiu na njaa kali ya kuajiriwa..Mungu kinusuru kizazi hiki cha wasomi wa Tanzania ambao wanasiasa watanzania wameamua kuwachomesha mahindi.
#MaendeleoHayanaChama
Sent using Jamii Forums mobile app
Hatari mnongumu sana
Tutajiajiri vipi na huku hatuna mtaji, mbaya Zaidi serikali haimtambui mwenye kipaji.Kwa masikitiko makubwa kwa vijana wanaosoma na wazazi kusomesha.
Jana nimeshuhudia wimbi kubwa la Majobless wa Leo na baadae. Ni baada ya kuhudhuria usaili wa kazi za kukusanya taarifa za makazi na postikodi.
Nafasi zilikuwa 415 tu kwa Manispaa ya Morogoro ila idadi ya waombaji ni 5500 hivi.
Sasa kwa uwiano wa waombaji na nafasi hata nusu haijafika, ni hatari mno.
Ushauri kwa vijana Wenzangu. Ni vyema kuondoa mawazo ya kuajiliwa na kupandikiza mawazo ya kujiajiri kwani kwa kutegemea ajira na hali iliyokuwepo unaweza ukakata tamaa ya maisha.
Kwenye elimu, Wazazi ni vyema ukamwambia mwanao mapema juu ya hatari ya kusoma elimu isiyo kuwa na ufundi ndani yake mfano ualimu na kazi nyingine.
Pia ni vizuri kuhamasisha watoto wetu kupenda shughuli halisi za jamii zetu kama kilimo na ufundi licha ya ukweli kwamba huko nako kunachangamoto lakini hutashindwa kuishi kupitia shughuli hizo. Ni Morogoro Manispaa me nimekosa kabisa imani ya kupata kazi yenyewe🙄🙄🙄
Kujiajiri kuna liability na kupata zaidi maana yake ni kujiongeza zaidi. Kumbuka kwenye kujiajiri jua na mvua vyote ni halali yako😅!Nenda mtaani Kama utakuta mtu amekaa idle tu. Sema Vijana tunahisi ajira ndo kazi rasmi pekee. Yaani mtu akiajiriwa alipwe laki 3 anaona ndo mwisho wa matatizo kuliko kujiajiri apate zaidi.
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Bora waishie meza kuliko wavunje na miguu kabisaKujiajiri kuna liability na kupata zaidi maana yake ni kujiongeza zaidi. Kumbuka kwenye kujiajiri jua na mvua vyote ni halali yako[emoji28]!
Ukiambiwa utafute 1.5M kwa mwezi kwa kujiajiri ukiwa kama Jobless ambaye huna hata tsh.100 ya mtaji unafikiri itakuchukua muda kiasi gani? Siku hufungui biashara jua sikuhio huingizi hata tsh.100
Ila kuajiriwa jua na mvua ni juu ya boss wako wewe alimradi umesaini siku jua utapata 1.5M yako bila kelele kila ifikapo kati ya tarehe 27-30!
Ajira tamu mkuu hasa ikiwa na maslahi mazuri. Its less stressing kama biashara kwa mtazamo wangu. Biashara inakuwa relaxed ukiwa na mtaji mkubwa yani ndio utafaidi biashara ila kwa hii mitaji yetu ya laki 1 na nusu tutaishia kuuza pweza barabarani tu mwisho utimuliwe na migambo wavunje meza.
Wakikuvunja na miguu ndio kabisa washakutia kilema ukicheki matibabu yako juu yani dah😅Bora waishie meza kuliko wavunje na miguu kabisa
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Anaongelea kuganga njaa sio kujiajiri huyo😅Tutajiajiri vipi na huku hatuna mtaji, mbaya Zaidi serikali haimtambui mwenye kipaji.
~kala Jeremiah
Aseeee ni hatari mkuuMwezi wa 6 kontena lingine la graduates linaingia mtaani likiwa na kiu na njaa kali ya kuajiriwa..Mungu kinusuru kizazi hiki cha wasomi wa Tanzania ambao wanasiasa watanzania wameamua kuwachomesha mahindi.
#MaendeleoHayanaChama
Sent using Jamii Forums mobile app