AJIRA:- POLISI Yaendelea Kupuuza AGIZO la Amiri Jeshi Kwa Kuajiri Vijana wa Mitaani badala ya JKT

AJIRA:- POLISI Yaendelea Kupuuza AGIZO la Amiri Jeshi Kwa Kuajiri Vijana wa Mitaani badala ya JKT

Phillemon Mikael

Platinum Member
Joined
Nov 5, 2006
Posts
10,557
Reaction score
8,673
Katika Miaka ya karibuni kumeeibuka mmomonyoko wa maadili kwenye utumishi wa umma ...kati ya mambo yalioshauriwa ili kuondoa mmomonyoko huo ,ilikuwa ni kurudisha JKT ,kwa kuanzia miaka ya mwanzo ya 2000 ..iliamua JKT irudi kwa vijana wa kujitolea ...,Ambapo baadaye iliamuliwa kuwa vijana hao wanaopikwa kwa mwaka mmoja hadi miwili ..wawe ndio sufuria kwa ajili ya kuvuna ..Askari wa :-
JWTZ
USALAMA WA TAIFA
MAGEREZA
POLISI
ZIMAMOTO
WANYAMA PORI

Vijana wanaobakia hapo watakuwa wa akiba na wanaweza kuajiriwa na Kampuni ya JKT Ya summa na wengine kuna mjadala wa kuwasaidia wawe wakulima stadi kadiri ya mafunzo yao kwa kuwapeleka vijijini na kuwapatia nyenzo za kisasa..

JESHI La Polisi miaka yote ndio limekuwa kielelezo cha kuporomoka kwa maadili kuanzia kwa vijana kupokea rushwa ,kushirikiana na majambazi ..kutokamilika au kuiva kinidhamu na kiuaskari ...na ukakamavu kwa ujumla...,kati ya yanayosababisha hili ni wimbi kubwa la rushwa wakati wa kuajiri,kujuana ,undugu..hasa unaohusisha kupendelea watoto wa LINE hata kama hawana sifa ..au wazazi wengine kufanya polisi ni mahali au jalala la kutupa watoto wao walioshindikana.

Tayari vikosi vya ulinzi na usalama vinachukua vijana JKT ikiwamo idara ya wanyama pori ambayo mwaka huu tu imechukua vijana 1,300 ...kila mwaka JKT inazalisha vijana 5000 kwa ajili ya soko la ajira ya vyombo vya ulinzi na usalama. Vijana hawa wameiva sana na wakipatiwa mafunzo ya Polisi pale moshi ya miezi 9 huwa bora na huwezi kulinganisha na kijana aliyookotwa maskani au kula kulala .

Wabunge wamepiga kelele sana juu ya Polisi kuendelea kupuuza agizo la AMIRI JESHI MKUU alilolirudia mwaka huu pale uwanja wa Taifa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya jkt...kulitaka liendelee kuwa kisima cha kupika askari..
LEO POLISI IMETANGAZA AJIRA ZAO NA KAMA KAWAIDA YAO WAO NDIO PEKEE WAMEENDELEA KUTOPITISHIA AJIRA JKT AU KUWATAKA WAOMBAJI WAWE WAMEPITIA MAFUNZO YA JKT......DHARAU ILIYOJE? WANAJUWA WAKIPITISHA HUKO HAWATAWEZA KUVUNA PESA ZA RUSHWA ZA AJIRA AU KUPITISHA WATOTO WAO MATEJA WALIOWASHIDWA KUWATUPA POLISI..AIBU!!! NA HASARA KWA TAIFA LINALOTUMIA MABILIONI KUANDAA VIJANA KWA NI NJEMA AMBAO POLISI WANAKWEPA KUWATUMIA
 
mitaa haina vijana, wote ni watanzania, wana haki sawa ya kuitumikia nchi yao.
 
Mtoa hoja ana hoja muhimu.Ni vizuri kuhakikisha wale wote wanaotaka kuingia kwenye mfumo wa vyombo vya usalama wapitie JKT.Wawe screened huko.Siku hizi kupata hata hizo ajira za polisi ni dili.
 
Hapana kwa hali ilivyo bora waajiriwe vijana wa JKT na sio vijana wasiojulikana maadili yao lakini pia mtu aliyepita JKT alafu akapata Police training atakuwa level nyingine kiukakamavu na nidhamu ya kiuaskari.
 
Ukumbuke kwamba hao vijana wanaopitia JK wengi wao wanaendelea na masomo ya elimu ya juu, kwa hiyo siyo rahisi kabisa wanaobaki watoshe kujiunga na POLISI, JWTZ na USALAMA wa taifa.
 
Hapana kwa hali ilivyo bora waajiriwe vijana wa JKT na sio vijana wasiojulikana maadili yao lakini pia mtu aliyepita JKT alafu akapata Police training atakuwa level nyingine kiukakamavu na nidhamu ya kiuaskari.

Ndiyo kwanza vijana wameanza kwenda JKT, Je ajira zisubiri wawe wengi? na je wenye sifa za kuendelea masomo ya juu wasiende kwa sababu tu etu wanatawakiwa kupewa kipaumbele
 
Jichola3 sio wote wanaoenda jkt wanaenda vyuoni..kumbuka hii ya kwenda vyuoni imeanza mwaka huu..miaka ya nyuma kuna vijana kibao walienda jkt na wako mtaani
 
Last edited by a moderator:
Ukumbuke kwamba hao vijana wanaopitia JK wengi wao wanaendelea na masomo ya elimu ya juu, kwa hiyo siyo rahisi kabisa wanaobaki watoshe kujiunga na POLISI, JWTZ na USALAMA wa taifa.


Kaka inawezekana ulikuwa hujuwi kuwa JKT imerudi toka miaka ya 2000 ..kwa vijana wa kujitolea ..na mwaka huu ndio imrudi kwa mujibu wa sheria..
HAPA TUNAONGELEA VIJANA WA KUJITOLEA AMBAO NDIO KUNA PRESIDENTIAL ORDER KUWA WAWE KWENYE STREAM YA KUINGIA KWENYE SECURITY ARGENCIES ...[PRIORITY]
 
"Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza."
 
Agizo lenye halikutolewa na rais isipokuwa wahusika walisema watalijadili waone uwezekano wa kulifanyia kazi sasa wewe umechanganya madesa.
 
Kaka inawezekana ulikuwa hujuwi kuwa JKT imerudi toka miaka ya 2000 ..kwa vijana wa kujitolea ..na mwaka huu ndio imrudi kwa mujibu wa sheria..
HAPA TUNAONGELEA VIJANA WA KUJITOLEA AMBAO NDIO KUNA PRESIDENTIAL ORDER KUWA WAWE KWENYE STREAM YA KUINGIA KWENYE SECURITY ARGENCIES ...[PRIORITY]
Hiyo presidential order ni namba ngambi ya mwezi wa ngani?
 
Ukumbuke kwamba hao vijana wanaopitia JK wengi wao wanaendelea na masomo ya elimu ya juu, kwa hiyo siyo rahisi kabisa wanaobaki watoshe kujiunga na POLISI, JWTZ na USALAMA wa taifa.

JKT imeendelea kuchukua vijana kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na sekta mbalimbali kila mwaka tangia mwanzoni mwa 2000s, kilichofanyika sasahivi ni kuweka sheria ya kuwalazimisha wahitimu wote wa kidato cha sita kupita JKT kwanza kabla ya kuingia vyuo vya elkimu ya juu.

Wapo vijana wengi sana ambao walijiunga JKT wakitokea mitaani walikokuwa hawana shughuli za kueleweka za kufanya lakini JKT ikawachukua na kuwapatia mafunzo na wao wakajitolea kulitumikia taifa wakiwa JKT kwa muda wa mwaka mmoja hadi miwili, na wengine hata miaka mitatu. Mimi binafsi ninawafahamu vijana wengi tu ambao wameapata ajira JKT kwenyewe, JWTZ na Wanyama Pori wakitokea katika mafunzo ya JKT.

Kwahiyo hoja ya msingi hapa ni kwa jeshi la polisi kuacha kuajiri vijana moja kwa moja kutoka mitaani bali wawatumie vijana waliojitolea kuingia JKT na wamefundishwa vizuri ukakamavu na nidhamu yao ni nzuri tofauti na hawa wa sasa wanaoajiriwa wengine walikuwa vibaka mitaani lakini kwakuwa wazazi wao au walezi wao wanaweza kutoa rushwa basi wanajikuta ndio wameajiriwa na hao ndio chanzo na sababu ya kuporomoka kwa maadili ya polisi.

Tunakumbuka hivi karibuni waziri wa mambo ya ndani Dkt Nchimbi alisema kuwa kwa mwaka jana tu jeshi la polisi limewafukuza kazi askari wapatao 172, na wanachelea sana kuendelea kutoa adhabu ya kuwafukuza kwakuhofia kuongeza majambazi huko mitaani. Idadi hii ya askari 172 kufukuzwa polisi kwa mwaka mmoja tu ni kubwa sana na inaonyesha ni kwa kiasi gani kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa askari wa jeshi la polisi nchini.

Bila kubadili utaratibu wa ajira kwa askari wa jeshi la polisi wala tusiatarajie kuona maboresho yoyote yenye tija ndani ya jeshi la polisi kwakuwa kama wanaoajiriwa wenyewe ndio hao waliokwisha washinda wazazi wao tusitarajie kuwa mafunzo ya miezi tisa ya ccp yanaweza kuwabadilisha, sana sana wanakwenda kuongeza ujuzi wa kutumia bunduki na wanaporudi vituoni kwao ndio wanakuwa wapangaaji wa njama za kufanya ujambazi.
 
Hiyo presidential order ni namba ngambi ya mwezi wa ngani?

Unajuwa AMRI YA RAIS? Maagizo anayo yatoa rais iwe hadharani au vikaoni hayo ndio tunaita Presidential decree....[ndio maana hotuba za rais huandikwa na kuutafitiwa kwa kuwa hatakiwi kuongea tu lolote kama mimi na wewe....] Maagizo anayoyatoa ni amri halali kabisa na akirudi ikulu wasaidizi wake wana kazi ya kuandika hayo maagizo kwenye maandishi na kupekeka kunako husika ....kimaandishi.

Hili suala la kupitishia ajira zote za vyombo vya ulinzi na usalama ni AGIZO LA RAIS NA AMIRI JESHI MKUU...nchi imekuwa ikitumia pesa nyingi sana ....[wengi hapa mnachanganya na hawa vijana wa mujibu wa sheria wakati kuna vijana wa Kujitolea 5,000 wamekuwa wakizalishwa JKT kila mwaka toka miaka ya 2000..hadi sasa]........hawa ndio wanatakiwa kuwa intergrated kwenye system.

Wameshapikwa miaka miwili ...hata siku moja hawawezi kufanana na hawa watoto wanaochukuliwa mitaani kwa kuwa hawana kazi ...MTU ANAYEONA MWANAYE HANA KAZI AENDE POLISI ....AMPELEKE KWANZA JKT MIAKA MIWILI ASOTE NA KUCHUJWA ...NDIO AINGIE POLISI...SIO KUWA NA DOUBLE STANDARD WENGINE WANACHUKULIWA MITAANI WENGINE WANAPITA KUSOTA JKT ILI WAAJIRIWE......POLISI INAWAVUNJA MOYO SANA!!
 
Agizo lenye halikutolewa na rais isipokuwa wahusika walisema watalijadili waone uwezekano wa kulifanyia kazi sasa wewe umechanganya madesa.
JKT Iendelee kuzalisha vijana kwa ajili ya jeshi,idara ya usalama ,polisi …..[rais Kikwete ,Jul 10 ,2013, uwanja wa uhuru ..maadhimisho ya miaka 50 ya jkt]

Wizara ya Ulinzi imeamua kutumia utaratibu wa kuajiri vijana wanaotaka kujiunga na vyombo vya ulinzi na usalama kutoka kwenye JKT na JKU ili kupata vijana ...[ministry of defence]

43. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/2012, Jeshi la Polisi limeajiri askari wapya 3,264. Katika mwaka 2012/2013, Jeshi la Polisi linatarajia kuajiri askari wapya 3,000. Sehemu ya waajiriwa itapatikana kutoka katika mashule na vyuo vya elimu ya juu na idadi nyingine kutoka vijana wa JKT. Utaratibu huu unalenga kuwa na askari wenye sifa stahiki na waaminifu kwa kazi ya Polisi.[ hansard Bunge 2013]

Katibu Mkuu Kiongozi ,Ombeni Sefue ametaka Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Kutoa Kipaumbele cha ajira kwa JKT ..kwa kuwa inazalisha vijana wazalendo ,wakakamavu na waliopikwa……..[habari leo]
http://www.m.habarileo.co.tz/index....3784-ataka-jkt-wapewe-kipaumbele-katika-ajira


ANKO DEO NIMEKUWEKEA MFULULIZO MBALI MBALI WA HAYA MAAGIZO KUANZIA KWA RAIS ,KATIBU MKUU kiongozi[ambaye pia ni mjumbe kwenye NSC],,Waziri wa ulinzi ,Waziri wa Mambo ya ndani etc....

UKIANGALIA HOTUBA YA NCHIMBI[REFER HANSARD] ..
KATIKA KUKABILIANA NA HII HALI YA MMOMONYOKO ....HILI SUALA LA AJIRA ALIAHIDI BUNGENI KAMA KUWA AJIRA ZA POLISI ZITAPATIKANA MAENEO YAFUATAYO..
1.DIRECT recruitment kutoka vyuoni ..especially kwa askari wanaohitaji kuwa na fani kama sheria ,udaktari ,etc
2.DIRECT recruitment kutoka JKT

HAKUNA MAHALA KWENYE HOTUBA YAKE NCHIMBI ALISEMA WATATANGAZA KUOKOTEZA WAAJIRIWA MITAANI ...KAMA AMBAVYO SASA POLISI WANATAKA KUFANYA.....
NI WAZI KUWA AJIRA ZA JESHI ZA POLISI ZINAZOPITIA KIHOLELA NI SOURCE KUBWA SANA YA RUSHWA ZA AJIRA ....NA WANAJUWA WAKIFANYA KAMA WAZIRI ALIVYO AHIDI KUCHUKUA DIRECT TOKA VYUONI[WATAALAMU] AU JKT..HUKO HAKUNA KUTOA CHOCHOTE.

PIA LAZIMA MUELEWE KUWA HATA WASOMI WAPO WANAOJITOLEA KUTUMIKA JKT MIAKA 2 ILI WAAJIRIWE NA MWAKA HUU PEKEE WENYE DEGREE YA KWANZA NA YA PILI WAPO 210 WALIMALIZA MIAKA MIWILI ...NA RAIS ALIAGIZA WAWE INTERGRATED HARAKA....
POLISI WAAACHE KUAJIRI KWA KUJUANA NA RUSHWA....!!
 
Mleta mada umekurupuka sana. kama ungejua jinsi jkt wanavyotoa nafasi kwa ubaguzi na upendeleo usingeongea suala hili. Vilevile vijana wote waliopo jkt wanamalengo ya kuingia jwtz hivyo wakichukuliwa polisi au magereza wanakua na nidhamu mbovu na kudharau kwa kusema polisi au magereza jeshi gani hili lisilo na maslahi. Hii ni mbaya sana.. Mfano polisi na magereza mbona wanachukua sana vijana wa jkt.Tambua jkt kama hauna mzazi au ndugu mwanajeshi huwezi kupata nafasi hata siku moja.

Polisi wanajitahidi kutumia mfumo wa kisasa kuajili wanafunzi moja kwa moja kupitia mashuleni na kujaza fomu ukiwa chuoni. Mfano mwaka jana jeshi la magereza katika nafasi 1000, vijana 500 walichukuliwa jkt na 500 wengine walitoka uraiani. USIWE MTU WA KUTOKWA MIPOVU NA KUKURUPUKA KAKA. Tambua asilimia 98% ya vijana wa jkt hawapendi kuajiliwa magereza na polisi, hivyo waacheni polisi na magereza wachukue vijana uraiani.
 
Mleta mada umekurupuka sana. kama ungejua jinsi jkt wanavyotoa nafasi kwa ubaguzi na upendeleo usingeongea suala hili. Vilevile vijana wote waliopo jkt wanamalengo ya kuingia jwtz hivyo wakichukuliwa polisi au magereza wanakua na nidhamu mbovu na kudharau kwa kusema polisi au magereza jeshi gani hili lisilo na maslahi. Hii ni mbaya sana.. Mfano polisi na magereza mbona wanachukua sana vijana wa jkt.Tambua jkt kama hauna mzazi au ndugu mwanajeshi huwezi kupata nafasi hata siku moja. Polisi wanajitahidi kutumia mfumo wa kisasa kuajili wanafunzi moja kwa moja kupitia mashuleni na kujaza fomu ukiwa chuoni. Mfano mwaka jana jeshi la magereza katika nafasi 1000, vijana 500 walichukuliwa jkt na 500 wengine walitoka uraiani. USIWE MTU WA KUTOKWA MIPOVU NA KUKURUPUKA KAKA. Tambua asilimia 98% ya vijana wa jkt hawapendi kuajiliwa magereza na polisi, hivyo waacheni polisi na magereza wachukue vijana uraiani.

Mambo mengi Uliyoandika hapo Juu yanahitaji utafiti kuweza kuyahalalisha ...mfano..Umesema vijana wengi waliojotolea JKT Wanataka kuingia JWTZ ( sio Polisi,magereza,fire,pori, au usalama ) ....ULIWAPA QUESTIONAIRE ..?
UNAWEZA KUDHIBITISHA VIPI KUWA MASLAHI YA POLISI NA MAGEREZA NI MABAYA KULIKO JWTZ...MAZINGIRA MAGUMU YA KAZI JE ??? kazi zote za ULINZI na usalama nchini mazingira na maslahi hayatofautiani sana ....Tofauti iliyopooo ni dhahiri kuwa Polisi wanakutana na wananchi Kila Siku na hata TAASISIS Kama Takukuru ..wamewataja Kama moja ya maeneo yanayoongoza kwa rushwa...mfano Traffic ,idara ya upelelezi etc....ni tofauti kabisa na wenzao wanaoshinda maporini.

MIMI SITOKI POVU ...LABDA KINYUME CHAKE....WEWE NIMEKUWEKEA NUKUU YA HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ...ALITAJA NJIA MBILI ZA KUPATA AJIRA ..1.direct entry from college ( kujaza fomu especially kwa fani maalum) 2. direct entry from jKT ( volunteers ). Hakuna mahali ALIPOSEMA kwenye hotuba yake kuwa utaratibu ...uliojaa rushwa wa kuajiri mitaani utakuwa mmoja wapo utakaotumika kwa mwaka ..huu wa fedha ....( refer kwa kashfa ya rushwa ya ajira Makao makuu Polisi ikiratibiwa na "kamishna " Chalamila ( yahaya)....NYUMA yake wakiwa wakubwa Kibao aw kitengo cha UTAWALA .....ambapo vijana wengi sana ikibidi mwaka Juzi warudishwe kutoka CCP kwa kubainika walikuwa kwenye mtandao ulioingizwa kwa rushwa ....na wengi wakiwa na vyeti Vya kughushi
 
I need to research on this then nitapata cha kuchangia kwanini polisi wamechukua awamu zote tatu mtaan I .e wamefanya usaili kwa graduate, form four na form six pamoja na usaili wa watu wenye ujuzi mtaani.
 
Nina mashaka na upeo wa wachangiaji wengine, tukae tukumbuke hata hiyo nafasi ya kujiunga jkt tokea huo mwaka 2000 huwa haipatikani kirahisi eti kwamba ukiomba tu umepata, je lile kundi linalokosa hiyo nafasi hata ya jkt inamaana litaenda wapi? na kama jkt itakuwa ndio kipitishio cha hizo ajira kwa hali ya tanzania hao watoto wa vigogo watapata tu hivyo vyeti hata bila kuuzuria hayo mafunzo,pia sasa hv majeshi yetu yanabidi yawe ya kisasa je huko jkt kuna wataalam wa aina zote watakaoitajika?

JE, tukiitaji madactari 50 wenye degree waliopitia jkt watapatikana? mimi siamini kama uadilifu kama unatokana na mafunzo, ndio maana hata familia watoto wanakuwa na tabia tofauti ingawa wanapata malezi sawa, kama mtu ni mwizi ni mwizi tu, hata apitie huko JKT
 
unachosema ni sahihi mkuu,polisi wanaajiri vijana moja kwa moja toka mtaani tena wakati huo huo wanawachukua na baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo jkt...labda ni upungufu wa vijana wa jkt
 
Mkuu Phillemon Mikael hoja yako iko wazi tu sema kuna watu lazima wabishe na kutetea maslahi yao!!!!

Mtu anaposema eti vijana wengine watapata wapi ajira kama watachukuliwa waliopitia JKT moja kwa moja unaona upeo wa mtu huyu!!!!

Suala la usalama wa raia na mali zao lazima litazamwe kwa jicho la tatu ambalo ndio hili,likiletewa siasa,sijui fursa sawa kwa wote na mengine kama hayo basi tujiandae kusikia hii mambo ya majambazi kutumia sare za kikosi fulani!!!!

Mwisho ni hao hao wanaolalamika kuwa jeshi la polisi halifanyi kazi inayotarajiwa!!!!!!
JKT iwe sehemu ya pre-requisite ya ajira za vyombo vya usalama hata professionals wapite huko hoja ya kusema kuna upungufu sijui na nini na nini ni udhaifu wa planning kwani inajulikana nani anastaafu lini kwa hiyo wajipange tu,mabadiliko chanya hayaji kama mvua!!!
 
Back
Top Bottom