AJIRA:- POLISI Yaendelea Kupuuza AGIZO la Amiri Jeshi Kwa Kuajiri Vijana wa Mitaani badala ya JKT

AJIRA:- POLISI Yaendelea Kupuuza AGIZO la Amiri Jeshi Kwa Kuajiri Vijana wa Mitaani badala ya JKT

uadilifu ni tabia ya mtu, kwani hata huko mbele walipoendelea kiusalama na uzalendo wanao enda kinyume wapo haijalishi mtu kapata mafunzo gani ndio maana tunaona mtu kama snowden anatoa siri, uzalendo na uadilifu si kitu kinachoweza kujengwa kwa miezi sita au mwaka
 
Katika Miaka ya karibuni kumeeibuka mmomonyoko wa maadili kwenye utumishi wa umma ...kati ya mambo yalioshauriwa ili kuondoa mmomonyoko huo ,ilikuwa ni kurudisha JKT ,kwa kuanzia miaka ya mwanzo ya 2000 ..iliamua JKT irudi kwa vijana wa kujitolea ...,Ambapo baadaye iliamuliwa kuwa vijana hao wanaopikwa kwa mwaka mmoja hadi miwili ..wawe ndio sufuria kwa ajili ya kuvuna ..Askari wa :-
JWTZ
USALAMA WA TAIFA
MAGEREZA
POLISI
ZIMAMOTO
WANYAMA PORI

Vijana wanaobakia hapo watakuwa wa akiba na wanaweza kuajiriwa na Kampuni ya JKT Ya summa na wengine kuna mjadala wa kuwasaidia wawe wakulima stadi kadiri ya mafunzo yao kwa kuwapeleka vijijini na kuwapatia nyenzo za kisasa..

JESHI La Polisi miaka yote ndio limekuwa kielelezo cha kuporomoka kwa maadili kuanzia kwa vijana kupokea rushwa ,kushirikiana na majambazi ..kutokamilika au kuiva kinidhamu na kiuaskari ...na ukakamavu kwa ujumla...,kati ya yanayosababisha hili ni wimbi kubwa la rushwa wakati wa kuajiri,kujuana ,undugu..hasa unaohusisha kupendelea watoto wa LINE hata kama hawana sifa ..au wazazi wengine kufanya polisi ni mahali au jalala la kutupa watoto wao walioshindikana.

Tayari vikosi vya ulinzi na usalama vinachukua vijana JKT ikiwamo idara ya wanyama pori ambayo mwaka huu tu imechukua vijana 1,300 ...kila mwaka JKT inazalisha vijana 5000 kwa ajili ya soko la ajira ya vyombo vya ulinzi na usalama. Vijana hawa wameiva sana na wakipatiwa mafunzo ya Polisi pale moshi ya miezi 9 huwa bora na huwezi kulinganisha na kijana aliyookotwa maskani au kula kulala .

Wabunge wamepiga kelele sana juu ya Polisi kuendelea kupuuza agizo la AMIRI JESHI MKUU alilolirudia mwaka huu pale uwanja wa Taifa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya jkt...kulitaka liendelee kuwa kisima cha kupika askari..
LEO POLISI IMETANGAZA AJIRA ZAO NA KAMA KAWAIDA YAO WAO NDIO PEKEE WAMEENDELEA KUTOPITISHIA AJIRA JKT AU KUWATAKA WAOMBAJI WAWE WAMEPITIA MAFUNZO YA JKT......DHARAU ILIYOJE? WANAJUWA WAKIPITISHA HUKO HAWATAWEZA KUVUNA PESA ZA RUSHWA ZA AJIRA AU KUPITISHA WATOTO WAO MATEJA WALIOWASHIDWA KUWATUPA POLISI..AIBU!!! NA HASARA KWA TAIFA LINALOTUMIA MABILIONI KUANDAA VIJANA KWA NI NJEMA AMBAO POLISI WANAKWEPA KUWATUMIA

utafiti unaonesha kuwa vijana wengi wanaotoka JKTni wavuta bangi,hata polisi wengine wanathibitisha kuwa polisi waliopitia JKT ndio wengi wanaofanya mambo ya ajabu kwa sababu katika mafunzo hayo ya JKT wanavutishwa njeve
 
"Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri vijana kutoka katika makundi yafuatayo: waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, kidato cha sita mwaka 2013, JKT/JKU mwaka 2013 na vyuo vya elimu ya juu mwaka 2013.Taratibu zinakamilishwa ili waliomaliza kidato cha nne na sita na waliojaza fomu za maombi kabla ya kumaliza mitihani yao ya mwisho waitwe kwenye usaili.

Usaili wa vijana wa JKT umekamilika mapema mwezi Aprili, 2013.Tangazo hili linawaalika vijana walioko kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini watakaohitimu masomo hivi karibuni na wanaopenda kujiunga na Jeshi la Polisi. Fomu za waombaji baada ya kujazwa kikamilifu ziletwe na mkuu wa chuo kabla ya tarehe 30/6/2013" , source website ya police
 
Nadhani watu wanachanganya mambo polisi wanachangacha watu kutoka sehemu mbalimbali ikiwepo na Jkt.
Kuna askari mmoja aliwahi kuniambia kuwa kwa tafiti zao askari wengi wanaotoka jkt ni wasumbufu sana hao wakosefu wa maadili uliowataja mtoa mada asilimia kubwa ni wa jkt hvyo polisi iliamua kutochukua askari wengi kutoka jkt.
 
Back
Top Bottom