AJIRA:- POLISI Yaendelea Kupuuza AGIZO la Amiri Jeshi Kwa Kuajiri Vijana wa Mitaani badala ya JKT

uadilifu ni tabia ya mtu, kwani hata huko mbele walipoendelea kiusalama na uzalendo wanao enda kinyume wapo haijalishi mtu kapata mafunzo gani ndio maana tunaona mtu kama snowden anatoa siri, uzalendo na uadilifu si kitu kinachoweza kujengwa kwa miezi sita au mwaka
 

utafiti unaonesha kuwa vijana wengi wanaotoka JKTni wavuta bangi,hata polisi wengine wanathibitisha kuwa polisi waliopitia JKT ndio wengi wanaofanya mambo ya ajabu kwa sababu katika mafunzo hayo ya JKT wanavutishwa njeve
 
"Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri vijana kutoka katika makundi yafuatayo: waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, kidato cha sita mwaka 2013, JKT/JKU mwaka 2013 na vyuo vya elimu ya juu mwaka 2013.Taratibu zinakamilishwa ili waliomaliza kidato cha nne na sita na waliojaza fomu za maombi kabla ya kumaliza mitihani yao ya mwisho waitwe kwenye usaili.

Usaili wa vijana wa JKT umekamilika mapema mwezi Aprili, 2013.Tangazo hili linawaalika vijana walioko kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini watakaohitimu masomo hivi karibuni na wanaopenda kujiunga na Jeshi la Polisi. Fomu za waombaji baada ya kujazwa kikamilifu ziletwe na mkuu wa chuo kabla ya tarehe 30/6/2013" , source website ya police
 
Nadhani watu wanachanganya mambo polisi wanachangacha watu kutoka sehemu mbalimbali ikiwepo na Jkt.
Kuna askari mmoja aliwahi kuniambia kuwa kwa tafiti zao askari wengi wanaotoka jkt ni wasumbufu sana hao wakosefu wa maadili uliowataja mtoa mada asilimia kubwa ni wa jkt hvyo polisi iliamua kutochukua askari wengi kutoka jkt.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…