Ajira Portal, Help Desk ni kero tupu!

Ajira Portal, Help Desk ni kero tupu!

Reality of heaven

Senior Member
Joined
Nov 2, 2022
Posts
108
Reaction score
353
Ajira portal kama hamuwezi kuwasaidia watu hamna haja ya kuwa na help desk, maana mtu anakuwa na shida anawapigia toka asubuhi mpaka jioni, simu ipo busy, na ikiita haipokelewi.

Kwanini msiajiri watu special kwa ajili ya kazi hiyo tu! Kama wanavyofanya mitandao ya simu!! Nyinyi ndo mnaoajiri kwa nini mnashindwa kuwa na watumishi wa kutosha kuwahudumia wananchi? Naomba mjitafakari hiki kitengo.
 
Customer care ama help desk 90% hazifanyi kazi labda tu za makampuni binafsi tena yawe ya wafanyabiashara. Serikali ni utumbo tu
 
Ni kweli hapa wame feli pakubwa sana... kuna shida sana kupata huduma kupitia huduma kwa mteja ya utumishi
 
Ajira portal kama hamuwezi kuwasaidia watu hamna haja ya kuwa na help desk, maana mtu anakuwa na shida anawapigia toka asubuhi mpaka jioni, simu ipo busy, na ikiita haipokelewi.

Kwanini msiajiri watu special kwa ajili ya kazi hiyo tu! Kama wanavyofanya mitandao ya simu!! Nyinyi ndo mnaoajiri kwa nini mnashindwa kuwa na watumishi wa kutosha kuwahudumia wananchi? Naomba mjitafakari hiki kitengo.
Pole sana, kwa nyongeza, hata hao wahuduku wa makampuni ya simu nafikiri wamepewa maelekezo wasiongee na mteja kwa zaidi ya dakika 5 sijui..ukiongea nao uwe umepata suluhisho au la, unaona anakomaa kukata simu upige tena. Wahudumu wa simu wa ukweli ni wa makapuni ya betting, hawa wapo vizuri sana.
 
Hivi kwanini wanataka certified copies badala ya cheti original?

Kuna sababu yoyote ya kitaalamu
 
Hivi kwanini wanataka certified copies badala ya cheti original?

Kuna sababu yoyote ya kitaalamu
Ww hili swali lako liko kila thread ya ajira portal,kwani tabu iko wapi uki certify ukaweka mkuu?

Kwani ku certify vyeti ni dhambi??

Wanataka kuepuka udanganyifu! Full stop.
 
Back
Top Bottom