Niende moja kwa moja kwenye point. Lengo la hii mifumo ni kurahisisha process ya kuomba ajira na kuongeza umakini katika kuhakiki taarifa za mwombaji. Kwenye mfumo mtu anawajibika kuupload copy za vyeti zilizokuwa certified. Kwanini mfumo usiwe intergrated na necta directly.
Kwanini sehemu ya vyuo isiwe intergrated na TCU iwe tu mtu kuingiza namba yake the rest system inamaliza.
Hakuna option ya kudelete, ukiupload ukufanya error yoyote inayohitaji kudelete hiyo option hakuna.
Slowness, kwenye kuupload na kudownload data system inalemewa kwanini hawajawaza kuiongezea uwezo?
Naamini haya mambo yanarekebishika kama mkiamua kuwapunguzia mzigo watumiaji wa system yenu.
Kwanini sehemu ya vyuo isiwe intergrated na TCU iwe tu mtu kuingiza namba yake the rest system inamaliza.
Hakuna option ya kudelete, ukiupload ukufanya error yoyote inayohitaji kudelete hiyo option hakuna.
Slowness, kwenye kuupload na kudownload data system inalemewa kwanini hawajawaza kuiongezea uwezo?
Naamini haya mambo yanarekebishika kama mkiamua kuwapunguzia mzigo watumiaji wa system yenu.
Huu mfumo unaratibiwa na watu wa aina gani? Kwanini mnazuia vijana wasiweze kurekebisha au kudelete academic qualifications walizoziweka?
Halafu mbona mkiandikiwa email hamjibu? Pia sehemu ya feedback mmeweka recaptcha iliyo case sensitive lakini wakati wa kuandika mmeweka automatic upper case kwahiyo muda wote inakataa.
Rekebisheni haya matatizo.
Mliyowahi kuapply kupitia mfumo wa ajira portal mlifanyaje mkafanikiwa maana mimi nagomewa.
Lakini pia kwenye kipengele cha academic qualification Hamna option ya kufuta qualification zingine msaada wenu jaman
Hivi kweli hiki chombo mhimu ya Ajira nchini kina Wabobezi wa IT?
Yaani Website yao Iko hovyo sana linapo kuja suala la ku apply. Website, appearance ina vutia kwa nje. Ila sasa ingia ndani ktk ku chakata taarifa, ni website ya hovyo!!
Inawezeka kabisa kutokana na poor design ya Website hii, vijana wengi wenye sifa wakawa wana kosa ajira kisa kuondolewa na mfumo mbovu automatically. Mfumo utamwambia hana sifa, haja timiza vigezo, nk ili hali vigezo vyote anavyo. Baadhi ya matatizo nili kumbana nayo leo.
Kuna ajira ni lazima uombe kupitia ajira portal cha ajabu ukisign in kwa app yao inagoma hapo hapo ukisign up inaandika invalid email address na kila mtu hii inamkumba.
Kiujumla sahivi huwezi kuaccess ajira portal na hapo deadline ya maombi unakuta ni after few days.
Huu ni mkakati wa maksudi tu ili watu wasiombe wawekane wenyewe kwa wenyewe hawa ma-IT wa serikali na wanaosimamia hizi app na tovuti walipaswa wawe wamefukuzwa kazi.
Wakuu naombeni msaada, kila ninapojaribu ku update picha naona ina load tu lakini haibadiliki.
Picha iliyopo sasa hivi niliiweka wakati nipo certificate, sasa haikuwa ya passport size ilikuwa ni picha ya kawaida tu ya photo shoot.
Kwa anaejua namna ya ku update picha nyingine naomba anisaidie maana kila nikijaribu inagoma, msaada wakuu tafadhali.
Hivi kwanini ajira portal wanabana sana system ya kuomba kazi utumishi yaani mtu ana vyeti vyote kaweka kwanini wasimpe uhuru wa kuapply tu na sio kuoverqualify yaani wanafanya maisha yanakuwa magumu kabisa mtaani wakati mtu ana uwezo kabisa wa kuomba lakini system walivyoibana sio poa kabisa.