Hivi kweli hiki chombo mhimu ya Ajira nchini kina Wabobezi wa IT?
Yaani Website yao Iko hovyo sana linapo kuja suala la ku apply. Website, appearance ina vutia kwa nje. Ila sasa ingia ndani ktk ku chakata taarifa, ni website ya hovyo!!
Inawezeka kabisa kutokana na poor design ya Website hii, vijana wengi wenye sifa wakawa wana kosa ajira kisa kuondolewa na mfumo mbovu automatically. Mfumo utamwambia hana sifa, haja timiza vigezo, nk ili hali vigezo vyote anavyo. Baadhi ya matatizo nili kumbana nayo leo.
Mfano 1. Nafasi za LGTI -Assistant Lecturers Accounting & Finance. Eti Qualifiaction ni Master's Degree in Law? Law na Accounting uka ona dunia gani?
Hawa jamaa wanaweza kuwa wana fanya makosa haya kwa makusudi ili watu washindwe ku apply na wachukue watu wao kimya kimya au part time wa chuo. Kwa kosa hili, kila ata kae omba hiyo kazi. System ita mjibu hana Sifa!!
Mfano 2. Post ime andikwa applicant Must be a holder of Master degree in Finance. Mtu mwenye Bachelor degree in Accounting & Finance na Master of Business Admninistration (Specialization : FINANCE) ila website yao ina mkataa eti hana vigezo. Hii ina onesha ni jinsi gani website yao ilivyo karirishwa!!
Mfano no 3. Ku search Key words ya Kazi haikubali. Ila inakubali tu key word ya Taasisi ina maana kama taasisi ina kazi 200 upitie page zote kuperuzi kazi 1 baada ya nyingine, kwa sababu heading za kazi ziko hidden. Ku apply ambako kunge tumia dk 30. Una tumia siku 1 hadi 2.
Mfano 4. Kuna tatizo la Backward. Mfano ume click Vacancies page 32. U click kusoma moja wapo ya kazi ktk page 32.e.g. row 1. Uki rudi nyuma kidogo ili uende row 2, kosa!!! Ina kutoa moja kwa moja toka page 32 hadi page 1 ya Vacancies(yaani home page ya Vacancies).
Kwani hawawezi kuandika openly Taasisi...then row 1 kazi namba 1 jina la kazi namba 1. Then, Row 2 kazi namba 2 jina lake...nk. ili mtu aende direct. Yaani wame fanya ku apply kazi nako kume kuwa kama kutafta kazi!! Unnecessary disturbances.
Mfano 5. Issue ya GPA. Una kuta kazi inataka 3.5 au 3.8 ila ww una 4.0. masters wana taka GPA ya 3.8 au 4.0 ila ww una zaidi ya hizo. Vyuo vingi vya nje Master's au PhD hawana mambo ya GPA ni Distinction, Credit au Pass (au A, B+, B-, C na Pass). Designer wa hii website na maboresho yake ina onesha yupo local sana. Hiyo ni kazi ya Recruitment committee siyo Website. Vyuo vinajua 3.5 to 3.9 ni equivalent na upper second class, nk.
Kwanza hiyo system nime ona haina huwezo wa kusoma GPA ktk vyeti. Hii kazi ifanywe na selection team.
Mfano 6. Kazi ni ya Rector II Financial Management-(ADEM). Requirements ni B. Education in Commerce, or Bachekor of Arts in related fields. Pia uwe na masters in related fields. Mtu una B. Arts in Business (Accounting &Finance) na MBA ( Finance) na ufaulu wote wa GPA unao. Mfumo una kwambia huna vigezo. Duuh. Hii portal ime kuwa designed na mtu local sana. Ili paswa Key words za Programme/Course ndio itumike ku screen. Sasa wao uta kuta wame limit Education!
Tuna omba kama kuna technical problems mseme pia na museme na mu extend application deadline na mrudishe kwenye default settings , Au kama na ninyi mmerecruit watu wasio na sifa ya kazi zao, nanyie mtangaze kazi zenu tuziombe upya. Deadline za kazi zinafika. Ila ku appy kuwezekani.