KERO Ajira portal ni tatizo, na huduma kwa wateja hakuna msaada

KERO Ajira portal ni tatizo, na huduma kwa wateja hakuna msaada

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari?

Mfumo wa AJIRAPORTAL umenizuia kuomba nafasi nyingi sana za kazi kutokana na mfumo wenyewe kushindwa kutambua namna Programs husika kwenye nafasi husika zinavyokuwa zimeainishwa. Lakini kupata msaada kwa help desk ya wahusika imeshindikana.

Emails hazibijiwi wala simu hazipokelewi. Lakini naomba kushauri programs ziandikwe kiusahihi na sio, kwa mfano; kuna tofauti kati ya Bachelor of Arts with Education (Linguistics and Kiswahili) na Bachelor of Education in Linguistics.

Wasiwe wavivu wakuandika wanaopakia hizo taarifa; wanatukosesha fursa. Mfano anaandika Bachelor of Education in Linguistics or Arts with Education (LINGUISTICS) huyo wa Arts with Education mfumo unamkatalia.

Na programs nyingine huandikwa kimakosa kabisa. Mfn, Bachelor degree with Education in Linguistics ndio kitu gani sasa?
 
Back
Top Bottom