Ajira sekta binafsi vs ajira za umma

Ajira sekta binafsi vs ajira za umma

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Observation hii nimeifanya kwa muda mrefu, nimeongea na watumishi waliojiriwa na kufanya kazi private sector Kisha wakajiriwa serikalini, waliofanya kazi maisha yao yote private sector na wafanyakazi waliojiriwa serikalini kisha wakajiriwa private sector na waliojiriwa na kufanya kazi maisha yao yote serikalini nilichojifunza na kukiona hiki.

1. Miaka ya mwanzo mnapoajiriwa private sector na serikalini, mfanyakazi wa private sector anakuwa na maisha mazuri zaidi na anafurahia maisha ya ajira

2. Inapofika miaka mitano kwenda mbele , mfanyakazi wa serikali ananza kupata raha ya kazi , wakati huo private sector anaanza kuichukia kazi (hapa sababu ni kupandishwa madaraja na ongezeko la mishara serikalini na wengi wafanyakazi wa serikali wanakuwa wamekaribia kumaliza Deni Leo la Kwanza alilokopa)

3. Inapofika miaka 10 na kuendelea , private sector wengi huwa wanajuta na kuwa na makasiriko mengi na upande wa pili wale wa serikalini wanakuwa wamegain momentum kwenye safari ya maisha, ( huyu private anagundua hana security, mshahara hauongozeki, hana fursa ya kuteuliwa au kupandishwa cheo, na upande wa pili huwa ni watu wenye kujiamini( job security ni kubwa, amepandishwa daraja, Kama yupo idara nzuri ameisha piga mipigo ya hela, deni la pili linakuwa limeisha, hapa anakuwa ametimiza tayari ndoto ya Mtanzania ya kuona mafanikio ni nyumba na gari, watoto wanasoma, kama alikuwa ni mjanja kamradi flani alikoanza tayari kanaenda na ana uwezo w kufinance, huyu wa private sector muda huo ananza kutafta matangazo ya ajira ya serikalini na wengine wanajikuta wamekosa vigezo shida umri.

4. Inapofika miaka 15 wengi wanakuwa Wana miaka 40 and above, kipindi hicho watumishi wengi huwa hawaoni fahari Wala hawajisifu kisa eti tu ni mfanyakazi (ukiambiwa life begins at 40 ndipo unaelewa huo msemo chanzo chake ilikuwa ni nini) kipindi hiki Kila binadamu hujikagua mwenyewe na kugundua amefanikiwa au bado, the same kwa wafanyakazi huwa hawaoni sifa sijui kumiliki nyumba na gari , kipindi hiki mada kubwa huwa ni ada za watoto wao, ni kipindi hicho ambacho wafanyakazi wa private sector huwa ni watu wenye makasiriko Sana, waoga mno kwa maboss wao , wengi huwa wanajuta Sana hapa kwa Nini sikuajiriwa serikalini, hapa ndipo wafanyakaz hata wa serikali huanza kuchukia kazi zao Tena na wengi huchukia kama hakuteuliwa au kupandishwa cheo, wengi hapa huchukia mfumo wa utawala na chama tawala kuona kama kimejaa rushwa hasa inapotokea vijana wadogo kwake wanapokuja kuwa boss wake kazini na hususani wana elimu sawa, hapa wafanyakazi wengine huacha kabisa kufuatilia Mambo ya nchi na siasa

5. Inapofika miaka 50 hofu huwa kubwa sana kwa wafanyakazi wote,private sector hujiona ni mtu mwenye mikosi, hakuchukua hatua stahiki kwenye maisha, wengi huwa wanaujiuliza Sana kwa Nini sikuacha kazi na kujiajiri mwenyewe?

Upande wa pili huwa pia ni watu wenye hofu Sana na wengi huwa wanajiuliza sana hapa hivi Niki stafu itakuwaje, hivi ntaishi wapi, hawa watoto wadogo bado wanasoma dah sijui ntasomeshaje ? Kiufupi wengi hapa huwa na watu wa ibada Sana

6. Miaka 55 (umri wa kustafu kwa hiyari) private sector huwa ni watu hatari sana hapa, akitazama umri wake, akitazama alichokifanya maishani, akijilinganisha na wafanyakazi wa serikali, akiwaza kiasi kidogo cha fedha (pension) Atakayopata baada ya kustafu, hiki kipindi ndicho wafanyakazi waliokuwa smart kimavazi, mentality yao huwa ni mbovu na wengi hujikuta wapo rafu eti haogopwi kufukuzwa

Upande wa pili serikalini Pia huwa ni wenye hofu sana na huwa ni wafanyakazi wenye nidhamu sana, ni kipindi ambacho ukiwa mkuu wa wilaya unaweza kwenda ofisini ukawacharaza viboko na bado watakusifu, wengi waliokuwa wanoko kwa wafanyakazi wenzao unoko unaisha wanabaki ni watu wa imani sana, wengi hapa hufikiria atatumia pension yake vipi? na wale ambao hawakujipanga huanza kufikiria miradi hii kulima, na kufuga , kununua gari ya biashara na duka na hujaribu kufanya hivyo na wanapochemka hujutia Sana, ni kipindi pekee ambacho kila mfanyakazi huwa ni msikilizaji mzuri, unaweza mshauri chochote na akakusikiliza, maisha ya utumishi ni safari ndefu na ngumu Sana, ni Safari yenye furaha kidogo na majuto mengi.

Ushauri wangu kwa vijana pambana sana kupata kazi serikalini, ukipata kazi pambana sana kuwa na kazi nyingine nje ya ajira yako na pambana Sana kipato cha nje ya ajira kiwe ni kikubwa kuliko kipato cha ajira, mlioko serikalini kopa sana na wekeza, maisha ni Safari na wewe ni msafiri safiri ukijua siku zote ajira haiwezi kukupa raha ya maisha, ila ajira inauwezo wa kukupa starting capital, usiache kazi kwa kutamani maisha ya wengine, uhuru na raha ya maisha ipo kwenye kujiajiri huko nako kuna changamoto zake, ntaleta uzi wake siku moja, uzi huu nii matokeo ya Mimi kufanya kazi private sector, sasa nipo serikalini miaka kama sita, na daraja langu E, nimeajiajiri kwenye kilimo na ufugaji na nafanya biashara ya mazao ya kilimo na mifugo.
 
Una ukweli fulani ila umeegemea upande wa hasi tu ukasahau upande wa chanya.
 
Umechambua vizuri kabisa.
  • Starting ya ajira zao
  • Katikati ya safari ya ajira zao
  • Mwishoni mwa safari ya ajira zao
Km kuna mtu anaweza kuchambua zaidi ya hapa it's okay. Lakini ujumbe umefika na upo very clear.

Ubarikiwe tu.
 
Yaani mtu kuajiliwa hususani serikalini yani ni kama ugonjwa fulani syndrome ya kutofikilia zaidi , imagine mtu baada ya mwaka anapadishwa dalaja na nyongeza ya sh 17,000 au 22000 anafurahi sanaa na kushangilia wakati gharama ya maisha inapanda mara tatu ya hapo.

Mgine, anakuambia kuna kupata pession ukistaafu loh!!!! Wakati hapo iko 25yrs anasubiri miaka 45 ili astaafu, hajui kwamba pession ni hera yake alio kua ana katwa na imewekewa riba ndogo ukilinganisha na price market, inaibiwa ila ana furahia kwa kukosa discipline ya kutunza pesa yake mwenyewe.

Imagine mtimishi kama mualimu anakatwa bima ya sh 70,000 kila mwezi wakati alipo hamna hospitali ya bima anasubiria augue sana ndo aende mkoani kutibiwa, manaake wanao faidi bima ni wajanja wa mjini anachangia watu yeye anafaidika kwa % ndogo tu.

Kwa ajiliwa private au serikalini ni utumwa na ujinga wakati nxhi yetu inafursa nyingi za ujasiliamali na kipato kipo juu juu, mimi labda unipe ajiliwe na UN au kupata ubunge uwazili wa commissioner ubalozi nk kwa lengo la kupiga pesa nipata mtaji ili nifungue biashara ya kimataifa.
 
Imebidi nisiumalize huu Uzi kwa sababu Ni batili, hivi utamringanisha mfanyakazi wa UN, GGM, North Mara Gold Mine, WHF, WHO ambaye Ana elimu nzuri/profession na watumishi wengi wa serikali?

Hao jamaa wanakula pesa nzuri bana na Wana uwezo wa kuamia sehemu nzuri nyingine
 
Una ukweli fulani ila umeegemea upande wa hasi tu ukasahau upande wa chanya.
Huyo jamaa anatupiga na kitu kizito vichwani, watumishi wa private wengi wao wanasukuma ndinga Kali Sana na mijengo mikubwa kuliko wengi wa serikalini (expect wabunge,mabalozi)

Na issue ya job security Ni upuuzi,Mimi Kama Nina gari zangu kuanzia tatu, Nyumba kuanzia tatu, mashamba hata matano na Bank pesa isiyo chini ya 40 millions Basi hata nikifukuzwa kazi private sitowaza maana ntapam Ana kutafuta nyingine huku nikiishi Maisha sawa au zaidi ya yule aliye serikalini.

Mimi Bado natamani nipate mchongo private sio serikalini
 
Yaani mtu kuajiliwa hususani serikalini yani ni kama ugonjwa fulani syndrome ya kutofikilia zaidi , imagine mtu baada ya mwaka anapadishwa dalaja na nyongeza ya sh 17,000 au 22000 anafurahi sanaa na kushangilia wakati gharama ya maisha inapanda mara tatu ya hapo.

Mgine, anakuambia kuna kupata pession ukistaafu loh!!!! Wakati hapo iko 25yrs anasubiri miaka 45 ili astaafu, hajui kwamba pession ni hera yake alio kua ana katwa na imewekewa riba ndogo ukilinganisha na price market, inaibiwa ila ana furahia kwa kukosa discipline ya kutunza pesa yake mwenyewe.

Imagine mtimishi kama mualimu anakatwa bima ya sh 70,000 kila mwezi wakati alipo hamna hospitali ya bima anasubiria augue sana ndo aende mkoani kutibiwa, manaake wanao faidi bima ni wajanja wa mjini anachangia watu yeye anafaidika kwa % ndogo tu.

Kwa ajiliwa private au serikalini ni utumwa na ujinga wakati nxhi yetu inafursa nyingi za ujasiliamali na kipato kipo juu juu, mimi labda unipe ajiliwe na UN au kupata ubunge uwazili wa commissioner ubalozi nk kwa lengo la kupiga pesa nipata mtaji ili nifungue biashara ya kimataifa
Unaweza kuwa sahihi kwa mtizamo wako ila kwa ground mambo ni mazito.

Maiti pale makaburi kinondoni au buguruni zingepewa nafasi ya kusema ndoto zao kabla ya kufa hakika UNGESHANGAA.

Uhalisia wa mambo unakuja baada ya kukua na kuanza kufikiria kwa kutumia experience na akili.
 
Back
Top Bottom