Ajira Serikali: Kwa tafsiri ya Serikali, ajira ni za walimu na watu wa afya pekee au?

Ajira Serikali: Kwa tafsiri ya Serikali, ajira ni za walimu na watu wa afya pekee au?

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
9,034
Reaction score
6,913
Habari zenu wadau.

Tangu nimeanza kusikia ishu ya kuwepo na tatizo la ajira nchi hii mara zote wanaozungumziwa kukosa ajira inaonekana ni watu wa sekta ya Elimu na afya.

Hii dhana miongoni mwa viongozi wa serikali inashangaza Sana, kwamba hata wanapotangaza kwamba wataajiri watu kadhaa basi huwa wanaajiri walimu na watu wa afya yaani manesi na madaktari.

Hili jambo la ubaguzi wa ajira nimeanza kuliona toka enzi za Mkapa na miaka yote hiyo hawa watu huwa hawana usaili wala nini.

Kwamba nyie watu wa serikali mnataka mtuambie kwamba vyuo vyote vikuu na vya Kati Tanzania hii vinatoa kozi za Ualimu na fani za afya tuu? Mbona kozi zingine ndio zina vijana wengi kuliko hizo kozi 2 mnazozipendelea?

Ifike mahala muelewe kwamba ajira ni pamoja na vijana waliosomea kozi tofauti na Ualimu na afya.Kila ajira zinazotangazwa huwa ni hao tuu kana kwamba fani zingine hawana shida ya ajira au mahitaji hayapo au wao wanapata Kazi kirahisi.

Binafsi nachukizwa sana na huu mtizamo wa serikali. Kama mnaona hizi fani zingine sio muhimu basi watu wote wasome Ualimu na mambo ya Afya na vyuo vifute hizo zingine msidahili vijana huko maana inaonekana serikali haijishughulishi na ajira zao.

Mtu atakwambia wajiajiri,kwamba usiposomea Ualimu na afya wewe unakuwa unaweza kujiajiri Ila hao mnaowaajiri kila tangazo wao ndio hawana uwezo wa kujiajiri? Hivi majuzi nilimsikia Waziri wa TAMISEMI bungeni akidai Halmashauri karibu zote hazina wahandisi zinatumia Technicians wachache waliopo na kwamba eti wataazima wahandisi kutoka JWTZ afu wawape kazi kwa mkataba. Nilishangaa Sana badala ya kuajiri unaazima huko, mbona basi msiwape Kazi kwa mkataba? Kwani mtaani hawako?

Kiukweli serikali inaniboa Sana na dhana finyu na ajira walionayo hao watu, si ajabu Prof Assad alikuwa sahihi kwa ile asilimia 60 ya wasio na uwezo.

Kama mnaona hamuwezi kuwaajiri basi wawekeeni mazingira rafiki ya wao kujiajiri au kuajiriwa na sekta binafsi. Kwa mfano Serikali huwa haikagui makampuni binafsi kuangalia kama haki stahiki za wafanyakazi zinafuatwa ikiwemo kima cha chini cha mshahara, mikataba ya ajira, mafao yao, kuwawezesha kwa mikopo, kuwapa tenda ndogo ndogo japo upendeleo kama inavyopendelea walimu na manesi nk.

Mathalani sekta ya ujenzi, zaidi ya 70% ya matumizi ya serikali huenda kwenye ujenzi sasa huko kuna wakandarasi na force account.Kwa wakandarasi kuna kipengele au takwa la kimkataba kwa Kampuni kuwa na mhandisi au Fundi Sanifu kwenye mradi lakini cha ajabu kampuni karibu zote zinawasilosha CV za kuiba ya hao watu lakini wakati wa utekelezaji wa Kazi hawapo bali wanatumia tuu yeyote awe fundi awe layman ili mradi wakwepe kulipa.

Mbaya zaidi wasimamizi wa mikataba hawafuati sheria kuhakikisha jambo hili linafuatwa maana hii ndio njia mojawapo ya kuwatengenezea ajira vijana kwenye fani ya ujenzi ambao serikali haiwaajiri. Hawa watu wangefuata sheria hao vijana wangepata ajira,wangepata mafao na Serikali ingepata kodi kwa njia ya PAYE. Sasa hivi Serikalini imekazana kusomesha vijana VETA sasa hao wakimaliza watajiajiri vipi wakati saizi kuna mafundi lundo mtaani na mambo hayaendi?

Kama Serikalini inashindwa kulinda maslahi ya watu wake basi iwaajiri yenyewe la sivyo basi vijana angalieni namna ya kuwa na jambo lenu, umachinga sio Kazi ndio maana mnadharaulika. Uhalifu na ISIS wakija kushamiri hapo baadae msije kusema hamjui chanzo.
 
Uhaba mkubwa wapi wewe,sasa kama ni hivyo mbona vyuoni fani tofauti na afya na elimu zina idadi kubwa ya vijana kuliko hizo 2?

Wote hao wakihitimu wanaenda wapi?
 
Kama jembe ni mali ya nini kusomesha watoto

Kumsomesha mtu siyo lazima maana iwe kupata kazi au ajira ya ofisini! Mantiki ni rahisi tu, hebu fikiria idadi ya wanaomaliza vyuo kila msimu na idadi ya nafasi za ajira zilizopo! Unaona vinaendana?

Kukusomesha ni kukupa elimu, na elimu ni upanuzi wa maarifa, fikira, ujuzi na stadi za kukusaidis wewe kuyamudu maisha yako hata ukiwa nje ya ajira rasmi! Ukidhani elimu ni lazima kuwe kuajiriwa na serikali basi endelea kusubiri kijana!
 
Naunga mkono hoja..

Lakini nafikiri hzo kada ndo zinaweza kua na mass employment.

Mf: Kituo cha afya, Manesi wanahitajika zaidi ya 15 wakati huo huo wanahitaji mhasibu mmoja dereva mmoja data clark mmoja ko kuna tofauti ya mahitaji.
 
Tuliwahi kuuliza swali kama hili hatukupatiwa majibu hadi leo. Wizara ya nishati, madini, ujenzi, mawasiliano, maendeleo ya jamii, fedha,maji, mifugo na kilimo nafasi za ajira mbona hazitolewi kwa mfuko huu,mbona hazitangazwi?

Mashirika kama tanesco,tpdc,ewura,Pura, bima,bot, tra, veta,puma, na kadhalika mbona hawatangazi nafasi za waliosome degree na kuendelea? Ukisikia nafasi imetangazwa ni nafasi ya mtunza kumbukumbu au katibu mhutasi.
 
Uhaba mkubwa wapi wewe,sasa kama ni hivyo mbona vyuoni fani tofauti na afya na elimu zina idadi kubwa ya vijana kuliko hizo 2?

Wote hao wakihitimu wanaenda wapi?
Vyuo vinafanya biashara. Havina mahusiano yoyote na kama utapata kazi au hutapata.

Ni jukumu lako kuamua utasoma nini.
 
Tuliwahi kuuliza swali kama hili hatukupatiwa majibu hadi leo. Wizara ya nishati, madini, ujenzi, mawasiliano, maendeleo ya jamii, fedha,maji, mifugo na kilimo nafasi za ajira mbona hazitolewi kwa mfuko huu,mbona hazitangazwi? Mashirika kama tanesco,tpdc,ewura,Pura, bima,bot, tra, veta,puma, na kadhalika mbona hawatangazi nafasi za waliosome degree na kuendelea? Ukisikia nafasi imetangazwa ni nafasi ya mtunza kumbukumbu au katibu mhutasi.
 
Kazi zipo nyingi tafuta cha kufanya kwani watu hawachomi mikaa na wakaishi?

Huko nyuma watu waliajiriwa na serikali ipi?

Amkeni uvuvi,uwindaji,uchoraji,uuhunzi,etc hizo ndiyo kazi za kudumu acha kubweteka
 
Tuliwahi kuuliza swali kama hili hatukupatiwa majibu hadi leo. Wizara ya nishati, madini, ujenzi, mawasiliano, maendeleo ya jamii, fedha,maji, mifugo na kilimo nafasi za ajira mbona hazitolewi kwa mfuko huu,mbona hazitangazwi?

Mashirika kama tanesco,tpdc,ewura,Pura, bima,bot, tra, veta,puma, na kadhalik mbona hawatangazi nafasi za waliosome degree na kuendelea? Ukisikia nafasi imetangazwa ni nafasi ya mtunza kumbukumbu au katibu mhutasi.

Kumsomesha mtu siyo lazima maana iwe kupata kazi au ajira ya ofisini! Mantiki ni rahisi tu, hebu fikiria idadi ya wanaomaliza vyuo kila msimu na idadi ya nafasi za ajira zilizopo! Unaona vinaendana? Kukusomesha ni kukupa elimu, na elimu ni upanuzi wa maarifa, fikira, ujuzi na stadi za kukusaidis wewe kuyamudu maisha yako hata ukiwa nje ya ajira rasmi! Ukidhani elimu ni lazima kuwe kuajiriwa na serikali basi endelea kusubiri kijana!
Bachelor of science in rural development, unakwenda kujiajiri au kuajiriwa? Degree zingine zipo tu ili malecturer wapate mishahara na kujiendeleza ili watape PhD
 
Upo sawa kabisa huu ni ubaguzi mkubwa sana, kada zote ni muhimu, haiwezekani kada ya ualimu au udaktari wachukuliwe watu kwa maelfu kwa mara moja then kuna kada nyingine watu elfu wanagombea nafasi moja, Tena nafasi zenyewe za msimu. Watanue goli nakada nyingine waweze kupata nafasi, hao waalimu na madaktari hawawezi kufanya kazi wenyewe.
 
"Umevaa shati la kujani na kofia yake"
Acha uchochezi hoka ya msingi hapa hao wazee wa zamani waliajiriwa na serikali ama waliishi kwa kazi zipi?

Kazi ni nyingi tu mtaani acha ubishoo.

Subiri sasa serikali ikupe ajira,mtu unakaa mjini ni tu unaenda shule eti unasubiri ajira,mwambie baba yako akupe akurithishe ajira yako.

Chuki hazikufikishi kokote hao ambao hawajasoma wanaishije?
 
Naunga mkono hoja..

Lakini nafikiri hzo kada ndo zinaweza kua na mass employment.

Mf: Kituo cha afya, Manesi wanahitajika zaidi ya 15 wakati huo huo wanahitaji mhasibu mmoja dereva mmoja data clark mmoja ko kuna tofauti ya mahitaji.
Sasa fani hizi tofauti na walimu ndio zina mass employment tofauti na jao manesi wanaajilowa wengi

Huo huoni Utumishi wakiitisha ajira 5 watu 1200 manake nini hii
 
Back
Top Bottom