Ajira Tume ya uchaguzi iangalie wanaosota mitaani badala ya kuajiri Walimu

Ajira Tume ya uchaguzi iangalie wanaosota mitaani badala ya kuajiri Walimu

pilau

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
1,595
Reaction score
451
Inasikitisha wakati kuna vijana wanahangaika mjini kutafuta ajira bila mafanikio ni dhahiri kwamba baada ya tangazo la tume ya uchaguzi kutangaza nafasi za kazi kwaajili ya uchaguzi mkuu wengi waliojitokeza kuomba ni waajiriwa tayari.

Wengi wao ni walimu na watendaji wa mitaa SERIKALI iliangalie hili wanaotakiwa kupewa upendeleo no wale vijana wanaosota mitaani walimu mlioajiriwa na waajiriwa wengine kuweni na HURUMA
 
Mwalimu naye anakwambia ana bills anatakiwa kulipa. Wacha wapambanie wote,, mshindi atashinda
 
Vijana msipende kulialia na kuonewa huruma. Ikiwa hao watumishi wa umma wana sifa stahiki waachwe waombe hizo kazi. Jobless wapendelewe?

Atakayepata na apate, then chapa kazi kwa uadilifu.
 
Wawape ili wapigwe na kitu kizito, thubutu yao kama wanajiamini
 
Nani ahangaike na jobless aache kuwapa watumishi wake anaowaamini?
 
kuwapa waalimu na watendaji ni lazima na muhimu kwa ushindi wa chama

nimesota miaka 8 leo unipe nafasi ya kusimamia nikuache utawale tena lazima juu chini nikuondoe

waalimu na watendaji ni maelekezo tu ya kuua wapinzani
 
Inasikitisha wakati kuna vijana wanahangaika mjini kutafuta ajira bila mafanikio ni dhahiri kwamba baada ya tangazo la tume ya uchaguzi kutangaza nafasi za kazi kwaajili ya uchaguzi mkuu wengi waliojitokeza kuomba ni waajiriwa tayari.

Wengi wao ni walimu na watendaji wa mitaa SERIKALI iliangalie hili wanaotakiwa kupewa upendeleo no wale vijana wanaosota mitaani walimu mlioajiriwa na waajiriwa wengine kuweni na HURUMA
Kama wewe ni mwalimu wa serikali omba hizo nafasi.....
Ila kama haupo kwenye sekta hiyo usijisumbue!
 
Ajira haitilewi Kwa huruma, ni Kwa anayedtahili. Pambana mkuu
 
Back
Top Bottom