Ajira za Sensa: Matapeli kazini

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
Hizi Ajira za Sensa ambazo sifa Ni nyepesi Sana. Hivyo waombaji watakua wengi itakayopelekea kuongeza ushindani. Tutarajie matapeli kuiltambaa na beat ili kuwapiga hao "makarani tarajali"

1. Tapeli anatumia Gmail.
2. Mchango @35,000 (malazi na chakula).
3. Picha je?

 
Wabongo noma.
Ila tarehe kachemka, inaonyesha mtambo ulitundikwa the day tu NBS wamefungua dirisha la maombi
 
Kwa hiyo Ngumbaru tutulie sio?
Mtego upo hapa:
1. Wamesema kuanzia elimu ya kidato cha nne, lakini wameweka mahali uchague elimu yako ni ipi, wakianzia ya chuo kikuu na kushuka hadi kidato cha nne

2. Wamesema ni kwa aliyeajiriwa na serikali, au binafsi au asiye na ajira (maana yake yeyote), lakini kuna mahali unatakiwa ujaze hali yako ya ajira, na kwa walioajiriwa unajaziwa na mwajiri sehemu yake

Mchujo upo, tena kwa software ni just kufanya sorting dakika moja tu wanabaki wanaodhaminika serikalini na wenye elimu kuanzia juu kushuka chini. Ni maoni yangu lakini, sina chanzo chochote
 
Wenyeviti wa CCM wilaya, wanawaambia vijana Kuna nafasi zimetengwa kwa wanachama wa CCM kwa hiyo ukikamilisha maombi nakala Moja unampelekea ukiambatanisha na 10,000. Jana mmoja alikuwa analewa pombe, kiti moto na mrembo pembeni. Huku muamala ukiendelea kusoma.
 
Patamu hapo
 
Afisa analewaaaa...
 
Hivi hawawezi kuwa track hao matapeli kupitia hizo info walizotoa ? maana sasa wamezidi

Halafu hawajiongezi tangu lini tangazo la kazi likawa na gmail
 
Kuna watu watatemwa na mfumo ila wataingizwa unajua kwa nini ?

Team ya wajumbe lazima waweke watu wao
 
Hawa jamaa wamezidi sasa hadi kero. Kwenye uchaguzi wa wabunge na rais walikuwepo na kitangazo chao, kwenye Corona wakawepo, uandikishaji wa nyumba na makazi kama kawa, wakaja na wanahitaji watu wa kukusanya ushuru kwenye majiji, sasa hivi hiyo sensa na kazi yao ni kuchonga tu mihuri na kufungua email mpya za gmail hii ni too much
 
Hivi wanashindwa kuwakamata kweli ?
 
Hapa Kuna mazuzu ya chama yatakuamini Kama imani ya dini. Halafu yataanza kusambaza hii stori mitaani kwa uhakika kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…