Mtu Kwao
JF-Expert Member
- Sep 2, 2019
- 394
- 720
Salaam...
Nipo jijini Dodoma yapata mwezi wa 2 Sasa lakini Kuna jambo linanishangazaa na kunisikitisha sana. Hapa mjini ajira za utotoni zimekithiri sana. Ukienda kwenye migawa hasa ya uswahilini unakuta asilimia kubwa watoto ndio Wana hudumia
Ukienda kwenye garage vilevile unakuta vitoto vidogo dogo ndo vinapewa kazi ya kufungua nati. Kwenye usafiri wa umma vile vile watoto ndo makondakta na wapiga debe stendi
Cha kushangazaa kabisa juzi nilienda kwenye taasisi moja ya elimu ya juu tena kubwa tu lakini nikashangaa kuona watoto wadogo ndio wanafanya usafi wa nje kufyeka na kufugia
Sasa ukitazama hao watoto kwa sura tu bado wadogo sana wanatakiwa kuwa mashuleni. Niiombe Serikali kuingilia kati suala hili ikibidi kuwachukulia hatua wote wanaowapa kazi watoto ambao Wanatakiwa kuwa shule
Hii ni kwa Dodoma sijajua na mikoa mingine kama hali hii ipo.