Ajira za utotoni zimekithiri Dodoma, Serikali iingilie kati

Ajira za utotoni zimekithiri Dodoma, Serikali iingilie kati

Kuna sehemu nilkuwa maeneo ya Manzese Dar. Hivi vitoto vidogo vichangu viko vingi kweli na vinaletwa kutoka mikoani kwa oda maalum. Ukikuta wakati ''vinapigwa mnada'' utashangaa sana. Utasikia waliyovileta wanapiga debe kabisa ''hii ni mali mpya imeingia leo hivyo bei yake ni tofauti''.
Kwahiyo wanunuzi wanaenda kuvifundisha kazi wenyewe?
 
Unajua kila nikipiga mahesabu Tanzania ya miaka 20 ijayo naona giza. Wanaume wengi vijana 10-20 years old ama ni machinga au bodaboda au jobless kabisa na wengine ni panya road. Wasichana ni machangudoa au ma-bar maid nk. Wakija kuchanya damu hawa watazaa mafisi-road na panya-road watakuwa cha mtoto. Hawa ndiyo wanaokuja kuifanya Tanzania isitawalike kabisa kama hatua hazitachukuliwa mapema.
ccm itajikaanga kwa mafuta yake... make kule ndo wamejazana
 
Salam...!

Nipo jijini dodoma yapata mwez wa 2 Sasa lakini Kuna jambo linanishangazaa na kunisikitisha Sana

Hapa mjini ajira za utotoni zimekithiri sana
Ukienda kwenye migawa hasa ya uswahilini unakuta asilimia kubwa watoto ndo Wana hudumia

Ukienda kwenye garage vilevile unakuta vitoto vidogo dogo ndo vinapewa kazi ya kufungua nati

Kwenye usafiri wa umma vile vile watoto ndo makondakta na wapiga debe stendi
Cha kushngazaa kabisa juzi nilienda kwenye taasisi moja ya elimu ya juu tena kubwa tu lakin nikashangaa kuona watoto wadogo ndo wanafanya usafi wa nje kufyeka na kufugia

Sasa ukitazama hao watoto kwa sura tu bado wadogo Sana Wanatakiwa kuwa mashuleni

Niiombe Serikali kuingilia kati swala hili ikibidi kuwachukulia hatua wote wanaowapa kazi watoto ambao Wanatakiwa kuwa shule

Hii ni kwa dodoma sijajua na mikoa mingine kama hali hii ipo..
Utashangaa serikali ipo na inalijua hili tatizo lakini wako bize tu kurogana na kuliibia taifa
 
Tuacheni mambo ya uzungu, 14 years ni muda muafaka wa kufanya kazi. Tulikuwa tukifanya kazi nzito za kifamilia enzi hizo katika umri huo, sasa leo the same thing haiwezi kushindikana.
Tulikuwa tunachunga wanyama, tunachanja kuni, tunalima, tunafua. Sasa what is the difference leo wakifanya kazi nyingine?
 
Hao siyo watoto wadogo bali ni maumbile yao! Tayari walikwisha maliza elimu ya msingi na sasa wako on job training.
Shule ya lazima ni form four. Usitetee ukiukwaji wa haki za watoto
 
Mimi napingana na wewe, serikali imeshindwa kupunguza umasikini na kutengeneza mifumo bora ya maisha kwa watu wake. Hao watoto wanafanya Kazi kwa sababu ya umasikini hawana wa kumtegemea sababu Hakuna mazingira wezeshi Ili wajimudu. Kwa hao wa magarage baadae ndio huwa mafundi wakubwa ikiwemo kuja kumiliki magarage na biashara za magari. Nani kakudanganya kwamba mfumo wa kwenda shule ndio jawabu la maisha.
 
Ni umasikini tu.Mzazi hawezi kumruhusu mtoto wake awe kijakazi(siyo mfanyakazi).Umasikini umetamalaki kule.Unayemuona mtoto ndiyo anatumikishwa ili aihudumie familia yake.
 
Shule ya lazima ni form four. Usitetee ukiukwaji wa haki za watoto
Kwa sheria ipi ya nchi hii? Elimu ya msingi inaishia darasa la sababu huo ulazima unatoka wapi?
 
Salam...!

Nipo jijini dodoma yapata mwez wa 2 Sasa lakini Kuna jambo linanishangazaa na kunisikitisha Sana

Hapa mjini ajira za utotoni zimekithiri sana
Ukienda kwenye migawa hasa ya uswahilini unakuta asilimia kubwa watoto ndo Wana hudumia

Ukienda kwenye garage vilevile unakuta vitoto vidogo dogo ndo vinapewa kazi ya kufungua nati

Kwenye usafiri wa umma vile vile watoto ndo makondakta na wapiga debe stendi
Cha kushngazaa kabisa juzi nilienda kwenye taasisi moja ya elimu ya juu tena kubwa tu lakin nikashangaa kuona watoto wadogo ndo wanafanya usafi wa nje kufyeka na kufugia

Sasa ukitazama hao watoto kwa sura tu bado wadogo Sana Wanatakiwa kuwa mashuleni

Niiombe Serikali kuingilia kati swala hili ikibidi kuwachukulia hatua wote wanaowapa kazi watoto ambao Wanatakiwa kuwa shule

Hii ni kwa dodoma sijajua na mikoa mingine kama hali hii ipo..

Maisha ya Dodoma ni magumu sana hao wanatafuta maisha
 
Bora hata hao.

Wilaya za Kahama na Nzega zimejaa watoto wa kiha chini ya miaka 15 wakitumikishwa kuchunga mifugo.

50%+ ya wafugaji wameajiri mchungaji muha na wengine warundi na 80%+ ni umri wa kuwa shule ya msingi.

Viongozi wa serikali za vijiji waliangalie hili kwa namna ya kipekee sana hasa huko Kigoma.

Ni bomu.
 
Tuacheni mambo ya uzungu, 14 years ni muda muafaka wa kufanya kazi. Tulikuwa tukifanya kazi nzito za kifamilia enzi hizo katika umri huo, sasa leo the same thing haiwezi kushindikana.
Tulikuwa tunachunga wanyama, tunachanja kuni, tunalima, tunafua. Sasa what is the difference leo wakifanya kazi nyingine?
Wewe ulikuwa unafanya Kaz za nyumban unasaidia lakin hawa wanafanya kwa ujira

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom