Ajira za utotoni zimekithiri Dodoma, Serikali iingilie kati

Mtu Kwao

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
394
Reaction score
720
Salaam...

Nipo jijini Dodoma yapata mwezi wa 2 Sasa lakini Kuna jambo linanishangazaa na kunisikitisha sana. Hapa mjini ajira za utotoni zimekithiri sana. Ukienda kwenye migawa hasa ya uswahilini unakuta asilimia kubwa watoto ndio Wana hudumia

Ukienda kwenye garage vilevile unakuta vitoto vidogo dogo ndo vinapewa kazi ya kufungua nati. Kwenye usafiri wa umma vile vile watoto ndo makondakta na wapiga debe stendi

Cha kushangazaa kabisa juzi nilienda kwenye taasisi moja ya elimu ya juu tena kubwa tu lakini nikashangaa kuona watoto wadogo ndio wanafanya usafi wa nje kufyeka na kufugia

Sasa ukitazama hao watoto kwa sura tu bado wadogo sana wanatakiwa kuwa mashuleni. Niiombe Serikali kuingilia kati suala hili ikibidi kuwachukulia hatua wote wanaowapa kazi watoto ambao Wanatakiwa kuwa shule

Hii ni kwa Dodoma sijajua na mikoa mingine kama hali hii ipo.
 
Kuna mitaa fulani pale Dom ukikatiza usiku unakuta vitoto havina chuchu wala siti eti nao vinauza...!

Lakini nadhani yote ni dalili za ugumu wa maisha!
 
Acha wafundishwe kazi usisubiri waje kuwa majambazi
Mimi nadhani huko ndiko kuwafanya waje wawe majambazi! Elimu sahihi ndiyo njia nzuri inayoweza kuwakomboa. Hivyo vibarua vya muda vitaisha au havitakimu mahitaji yao halafu wataingia mitaani kufanya ujambazi na umalaya.
 
Hizo ni stadi za kazi
 
Kuna mitaa fulani pale Dom ukikatiza usiku unakuta vitoto havina chuchu wala siti eti nao vinauza...!

Lakini nadhani yote ni dalili za ugumu wa maisha!
Kuna sehemu nilikuwa maeneo ya Manzese Dar. Hivi vitoto vidogo vichangu viko vingi kweli na vinaletwa kutoka mikoani kwa oda maalum. Ukikuta wakati ''vinapigwa mnada'' utashangaa sana. Utasikia waliyovileta wanapiga debe kabisa ''hii ni mali mpya imeingia leo hivyo bei yake ni tofauti''.
 
Hali ni ngumu sana...
Biashara ya watu hasa vitoto imekithiri sana!
 
Kwa hao walio garage hiyo nayo ni taaluma, huenda wameshindwa ku afford VETA and other formal schools waache hapo wajifunze. Wanazo ndoto zao hapo inasikitisha lakini acha wafanye kile wana afford kufanya.
 
Hali ni ngumu sana...
Biashara ya watu hasa vitoto imekithiri sana!
Unajua kila nikipiga mahesabu Tanzania ya miaka 20 ijayo naona giza. Wanaume wengi vijana 10-20 years old ama ni machinga au bodaboda au jobless kabisa na wengine ni panya road. Wasichana ni machangudoa au ma-bar maid nk. Wakija kuchanya damu hawa watazaa mafisi-road na panya-road watakuwa cha mtoto. Hawa ndiyo wanaokuja kuifanya Tanzania isitawalike kabisa kama hatua hazitachukuliwa mapema.
 
Kuna mitaa fulani pale Dom ukikatiza usiku unakuta vitoto havina chuchu wala siti eti nao vinauza...!

Lakini nadhani yote ni dalili za ugumu wa maisha!
Mtaa Gani Huo Mkuu
 
Kuna mitaa fulani pale Dom ukikatiza usiku unakuta vitoto havina chuchu wala siti eti nao vinauza...!

Lakini nadhani yote ni dalili za ugumu wa maisha!
Nimeishi Dom miaka minne sikuwahi kuiona hii.
 
Unapima umri kwa macho mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…