Ajira za utotoni zimekithiri Dodoma, Serikali iingilie kati

Sa si bora kuliko kuitwa ombaomba?
 
Kwahiyo wanunuzi wanaenda kuvifundisha kazi wenyewe?
 
ccm itajikaanga kwa mafuta yake... make kule ndo wamejazana
 
Utashangaa serikali ipo na inalijua hili tatizo lakini wako bize tu kurogana na kuliibia taifa
 
Tuacheni mambo ya uzungu, 14 years ni muda muafaka wa kufanya kazi. Tulikuwa tukifanya kazi nzito za kifamilia enzi hizo katika umri huo, sasa leo the same thing haiwezi kushindikana.
Tulikuwa tunachunga wanyama, tunachanja kuni, tunalima, tunafua. Sasa what is the difference leo wakifanya kazi nyingine?
 
Hao siyo watoto wadogo bali ni maumbile yao! Tayari walikwisha maliza elimu ya msingi na sasa wako on job training.
Shule ya lazima ni form four. Usitetee ukiukwaji wa haki za watoto
 
Mimi napingana na wewe, serikali imeshindwa kupunguza umasikini na kutengeneza mifumo bora ya maisha kwa watu wake. Hao watoto wanafanya Kazi kwa sababu ya umasikini hawana wa kumtegemea sababu Hakuna mazingira wezeshi Ili wajimudu. Kwa hao wa magarage baadae ndio huwa mafundi wakubwa ikiwemo kuja kumiliki magarage na biashara za magari. Nani kakudanganya kwamba mfumo wa kwenda shule ndio jawabu la maisha.
 
Ni umasikini tu.Mzazi hawezi kumruhusu mtoto wake awe kijakazi(siyo mfanyakazi).Umasikini umetamalaki kule.Unayemuona mtoto ndiyo anatumikishwa ili aihudumie familia yake.
 
Shule ya lazima ni form four. Usitetee ukiukwaji wa haki za watoto
Kwa sheria ipi ya nchi hii? Elimu ya msingi inaishia darasa la sababu huo ulazima unatoka wapi?
 

Maisha ya Dodoma ni magumu sana hao wanatafuta maisha
 
Bora hata hao.

Wilaya za Kahama na Nzega zimejaa watoto wa kiha chini ya miaka 15 wakitumikishwa kuchunga mifugo.

50%+ ya wafugaji wameajiri mchungaji muha na wengine warundi na 80%+ ni umri wa kuwa shule ya msingi.

Viongozi wa serikali za vijiji waliangalie hili kwa namna ya kipekee sana hasa huko Kigoma.

Ni bomu.
 
Wewe ulikuwa unafanya Kaz za nyumban unasaidia lakin hawa wanafanya kwa ujira

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…