Ajira za Utumishi wa Umma ziwe za mkataba wa muda maalumu kwa kada zote

Ajira za Utumishi wa Umma ziwe za mkataba wa muda maalumu kwa kada zote

Said Shagembe

Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
23
Reaction score
35
Ningepewa nafasi ya kuhudumu kama mwajiri ningebadilisha taratibu zote za UTUMISHI wa UMMA kutoka kuwa ajira za kudumu mpaka mkataba wa mwaka mmoja.

Naamini hakuna anaependa kutumika maisha yake yote, hivyo wanaochoka nafasi hizo wawaachie wale wanaozitaka.

Hii itaongeza chachu ya utendaji kazi uliotukuka kwani mwenye nia ya kusalia kazini Atafanya kazi kwa bidii na yule ambae Tayari ashajiweza kiuchumi na anatamani kufanya mambo yake binafsi, itakuwa ni muda sahihi kwake kutokuongeza mkataba na kufuata mambo yake. Nadhani hii itaondoa tatizo la ajira kwa kiasi chake.

Wapo watu wengi washazichoka kazi walizoajiriwa lakini wanaenda kwasababu tu ndiyo kazi zo na hii ndiyo hasa inafanya kuwepo kwa utendaji mbovu kwenye ofsini nyingi za Umma.

Nawasilisha.
 
Ajira za mikataba ya temporary na permanent zipo.

Ni ww kufungua huo Ubongo wako.

Kuna kazi ni za SIRI na si afya kubadirisha badirisha watendaji.

Pia kanuni za kiutumishi pamj na kupanda vyeo hutegemea ni muda gani umekaa ktk hiyo kada.

Kwa hilo unalosema unafkir utapata WAKURUGENZI / MENEJA wenye uzoefu ? Ikiwa kila mwaka unaweka intake mpya?
 
🤔 Inawezekana
Iko hivi, hata ikitokea ajira zikawa ni kama unavyoshauri hilo haliwezi kuondoa tatizo la ajira nchini kwa sababu kiwango cha nafasi za ajira kilichopo ni kidogo sana vs wanaotafuta ajira. Private sectors ni kama wanafanya hivyo kwa sababu wana mikataka kila mwaka but renewable. Kingine ni kwamba ajira ya muda mfupi hivyo haiwezi kusaidia kupata watu wenye experience, zamani serikalini ilikuwa ukiajiriwa baada ya miaka 2 ndiyo unapata confirmation maana wanakuwa wameweza kukupima utendaji wako kazini. Kumbuka serikalini pia walianzisha mfumo wa OPRAS ambao kila mwanzo wa mwaka mtumishi anawekeana malengo na mkuu wake wa idara na ikifika Disemba wote mnakaa na kufanya evaluation ya progress ili kama hujatimiza majukumu yako basi hatua stahiki zichukuliwe. Lengo lilikuwa zuri ili kuchuja na kuwaondoa wazembe kazini but sijui hata ilifia wapi. Ajira zitaongezeka kwa kuimarisha sekta binafsi kwa sababu ndiyo yenye uwezo wa kuajiri watu wengi. Mfano hebu cheki mtu kama Bakhressa kwa kampuni zake zote ameajiri watu wangapi? Waliojiajiri kwa kuuza bidhaa zake tuu ni wangapi? Angalia kampuni za Bia na soda zimeajiri watu wangapi huko mitaani kwenye groceries mabaa, maajenti wa vinywaji ni? Hii sekta ndiyo ilitakiwa serikali iilinde kwa wivu mkubwa na kuipa unafuu kwenye baadhi ya kodi ili ikue haraka na kutoa ajira nyingi .
 
Back
Top Bottom