Ajira za Utumishi wa Umma ziwe za mkataba wa muda maalumu kwa kada zote

Ajira kuwa permanent hakumaanishi huwezi kuacha kazi tena ni simple sana

Andika barua ya masaa 24 lipa na mshahara mmoja, au andika notisi ya mwezi mmoja bila kulipwa mshahara utaondoka kwa amani kabisa


Labda uniambie iwe hivyo kwa kigezo, cha kuhamasisha utendaji hapo kweli
 
Wazo zuri
 
Kwa mwaka Mmoja hamna.labda kama miaka mitano hapo sawa.kwa mwaka Mmoja huwezi kuwa mzoefu.mimi kama mwajiriwa natamani nikifikisha miaka mitano naachana na kazi ya kuajiriwa.Baada ya miaka mitano Lazima nikajiajiri niachane na huu utumwa wa kazi zenye ujira mdogo serikalini
 
unasema hivi sababu una kazi nikuulize swali kwanini wastaaf wengi wakitoka makazini wanafail life usiache kazi et unataka kujiajiri utapigwa virungu vya maisha mpaka unaona unachotaka kujiari haukionii wewe acha maneno ya vijiweni piga kazi mpk uzee wako mkuu
Na nature ya ubinadamu hakuna kazi ngumu kama kujituma mwenyewe mpk utumwe ndo maana matajiri wote wameunda strong management maana yake ile management imtume na imdirect mfano kama kina mond,mo, gsm nk ukiangalia management zao sio za kitoto sana
 
Ni utaratibu mzuri nadhani tukiandika katiba mpya tutakuja na Sheria za zingine kubadilisha mazoea

Sheria za kazi tulizo nazo ni outdated bado ni za mfumo wa kijamaa kubembelezana kwingi
 
Unataka watu waanze kuhonga hili wabaki makazini, na hizo gharama za usahili kila mwaka si bora zipelekwe mahospitalini au mashuleni, wazo zuri ila kieconomical haliko sawa
Na watu watahonga balaa🀣 itakuwa mfumo kama wa vibarua. Ukitaka kupangwa site unampa tip man selecta 😁
 
Ukiwa jobless ni sahihi kuwaza hvy, ila ukiwa na kazi huko serikalini huwezi kusema haya.
😁😁😁😁😁😁 Inaeleweka kuwa asilimia 90% ya waajiriwa serikalini hapa bongo wanahisi wamejikomboa kuipata check no.

Ni kama wametua mzigo wa mahangaiko ya kupata riziki zao za kila siku hivyo hawawezi na hawataki kusikia habari za kurudi mtaani.
 
Sahihi.
 
Kwa hiyo ma Daktari wa upasuaji wenye uzoefu wa miaka 20 kazini waondolewe alafu waletwe ma Junior waendeleze game
 
Kwa hiyo ma Daktari wa upasuaji wenye uzoefu wa miaka 20 kazini waondolewe alafu waletwe ma Junior waendeleze game
Kuna Cadre ambazo ni technical kweli zinahitaji wazoefu kama kada ya afya ila utaona pia hao watu hawafanyi kazi full time serikalini.

Kuna wanaofungua clinic zao binafsi na wengine huenda hudumia huko kama part time.
 
Mimi ninachopinga ni jitu limekaa serikalini mpaka limezeeka akili zimechoka, limekula Mishahara weee halijaridhika, eti limestaafu halafu linapewa mkataba wa miaka mfano miwili na serikali hiyo hiyo, hii mizee ndo inayozibia vijana nafasi za ajira, ifukuzwe yote waajiriwe vijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…