ajira za waalimu wapya

komekaone

Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
47
Reaction score
9
kwa mujibu wa gazeti la habari leo,naib wazir tamisemi anayeshughulikia elimu kassim majaliwa juz ametangaza ajira 26000 za walimu watakazomwagiwa walimu mwez januari mwakani. wakat huo huo mulugo akiwa bungeni siku chache nyuma alisema ajira hzo ni kuanzia february had march, wadau nisaidien hv hz ofis hazina mawasiliano au inakuwaje. sisi waalimu tunaosotea hzo ajira tumsikilize nani.
 
kwanza kumwagiwa ndio nini sasa hilo nalo udhalilishaji kwa kiwango cha juu kwa walimu. Poleni sana Walimu.
 
Mi mwenyewe sielewi elewi, maana wanatuchanganya.
 
Ukiwa unasubiri ajira ya serikali, jishughulishe na mambo mengine ya kimaenndeleo
 
Dah! mmoja anasema january mwingine anasema february/march na wote wanatoka serikali moja!!!
 
Imechapishwa Jumatatu, 23 Desemba 2013
00:04
Imeandikwa na John Nditi, Morogoro
Imesomwa mara: 2300
SERIKALI imetangaza kutoa ajira mpya 26,000 za walimu kuanzia Januari mwakani, ikiwa ni mpango endelevu wa kupunguza uhaba wa walimu katika shule za msingi na sekondari nchini.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mita (Tamisemi), anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa, alisema hayo juzi mjini hapa wakati akifunga kikao cha kazi cha siku tatu cha maofisa elimu wa mikoa na halmashauri za wilaya nchini, wanaosimamia elimu ya msingi.
“Serikali inatambua uhaba wa walimu na kila mwaka inatoa ajira mpya za walimu. Januari
2014 Serikali itatoa ajira 26,000 za walimu
wapya na maelekezo mengine yatafuata,“
alisema Majaliwa. Aliwataka maofisa elimu hao kuzingatia uwiano wa walimu wakati wa kuwapangia vituo vya kazi, badala ya kuendelea kuwalundika maeneo ya shule za mijini pekee. Pia aliagiza walimu hao watayarishiwe mazingira mazuri hasa katika maeneo ya pembezoni kwa kuwapatia motisha, ili kuwajengea moyo wa kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi katika vituo vyao vya kazi kwa lengo la kuwafanya wasikimbie vituo.
Licha ya kutangaza ajira hizo mpya, Majaliwa
pia alisema Serikali imetenga Sh bilioni 18 za
kutengeneza madawati yatakayosambazwa
shuleni na zabuni yake inatarajiwa kutangazwa mapema iwezekanavyo.
Alisema mpango huo unatarajia kuanza
mapema mwakani baada ya kumpata mzabuni, “najua kutokana na kiwango kidogo
cha fedha, hatutaweza kutosheleza, lakini huu
ni mwanzo.”
Aliwataka maofisa hao kujenga tabia ya
ufuatiliaji shuleni, ili kusimamia utunzaji wa
vifaa na wakikuta uzembe ni wajibu wao
kuchukua hatua ya kumaliza matatizo yaliyo
chini na uwezo wao.
Nitaamini pindi itakapotekelezwa, mawaziri wetu hutoa kauli zinazokinzana.
 
ndo maana TZ ilishinda kwenye maajab 7 ya ulimwengu
 
Unavigezo gani vya kusema kuwa MULUGO amekurupuka?? Huwezi jua KASIM majaliwa anaweza akawa wrong..mulugo akawa sawa/lolote laweza kutokea.
 
Mulugo yuko sahihi, we fuatilia ajira za walimu mwaka jana na mwaka juzi wote waliajiriwa katika kipindi hicho alichokitamka.
 
Hivi mulugo si ndo yule alisema Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zimbabwe au sio yeye nimemfananisha?
 
Kuna kila dalili za kusema ajira za walimu ni january...kwasababu serikali inataka ianze kwa sifa mpango wa BRN
 

Ajira ni mwezi wa kwanza ndugu, kama mfuatiliaji Mulugo alisema na vilevile alikuwa hana uhakika na anachoongea kuwa wanasubiri fungu kutoka TAMISEMI. Na sasa TAMISEMI waliokuwa wanasubiriwa kutoa fungu ndio hao washasema mwezi wa kwanza, Ila kwa hiyo taarifa mmeambiwa ajira zitatangazwa na mtasubiri kuambiwa utaratibu unaofuata. Nami nina swali ETI FEDHA ZA KUJIKIMU NI TSH NGAPI? Na maelezo ya waraka wa kiasi cha fedha za KUJIKIMU UNAPATIKANA WAPI???
 
Fedha za kujikimu inatokana na halmashauri utakayopangiwa mfano kwa manispaa ya morogoro..wanatoa laki tatu na sitini lkn kuna halmashauri nyingine wanatoa laki na sabini so haina garantee maalum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…