Imechapishwa Jumatatu, 23 Desemba 2013
00:04
Imeandikwa na John Nditi, Morogoro
Imesomwa mara: 2300
SERIKALI imetangaza kutoa ajira mpya 26,000 za walimu kuanzia Januari mwakani, ikiwa ni mpango endelevu wa kupunguza uhaba wa walimu katika shule za msingi na sekondari nchini.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mita (Tamisemi), anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa, alisema hayo juzi mjini hapa wakati akifunga kikao cha kazi cha siku tatu cha maofisa elimu wa mikoa na halmashauri za wilaya nchini, wanaosimamia elimu ya msingi.
Serikali inatambua uhaba wa walimu na kila mwaka inatoa ajira mpya za walimu. Januari
2014 Serikali itatoa ajira 26,000 za walimu
wapya na maelekezo mengine yatafuata,
alisema Majaliwa. Aliwataka maofisa elimu hao kuzingatia uwiano wa walimu wakati wa kuwapangia vituo vya kazi, badala ya kuendelea kuwalundika maeneo ya shule za mijini pekee. Pia aliagiza walimu hao watayarishiwe mazingira mazuri hasa katika maeneo ya pembezoni kwa kuwapatia motisha, ili kuwajengea moyo wa kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi katika vituo vyao vya kazi kwa lengo la kuwafanya wasikimbie vituo.
Licha ya kutangaza ajira hizo mpya, Majaliwa
pia alisema Serikali imetenga Sh bilioni 18 za
kutengeneza madawati yatakayosambazwa
shuleni na zabuni yake inatarajiwa kutangazwa mapema iwezekanavyo.
Alisema mpango huo unatarajia kuanza
mapema mwakani baada ya kumpata mzabuni, najua kutokana na kiwango kidogo
cha fedha, hatutaweza kutosheleza, lakini huu
ni mwanzo.
Aliwataka maofisa hao kujenga tabia ya
ufuatiliaji shuleni, ili kusimamia utunzaji wa
vifaa na wakikuta uzembe ni wajibu wao
kuchukua hatua ya kumaliza matatizo yaliyo
chini na uwezo wao.
Nitaamini pindi itakapotekelezwa, mawaziri wetu hutoa kauli zinazokinzana.