Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Serikali ya Ujerumani hapo jana umetia saini mpango wa kuwasajiri wakazi wasio katika Umoja wa Ulaya kwa lengo la kuziba pengo la wataalam katika sekta ya ajira.
Hatua hiyo inatekelezwa baada ya mkutano wa kilele uliowakutanisha wawakilishi wa makampuni na vyama vya wafanyakazi. Rasimu ya makubaliano iliyoridhiwa mwishoni mwa mkutano huo imetaja mipango ya kufuta ukiritimba sugu wa taratibu za Kijerumani na kulifanya taifa kuwa rafiki zaidi kwa wafanyakazi wa kigeni.
Mpango huo utatoa usaidizi kwa wafanyakazi wapya kupata mafunzo ya lugha ya Kijerumani, kutafuta eneo la kuishi. Na makampuni pia yatatoa nafasi zaidi za kazi zitakazo walenga wageni.
Serikali kwa upande wake imekubali kuongeza kasi ya kutoa viza kwa haraka ili kuwawezesha wafanya kazi kuanza majukumu yao haraka. Kwa hivyo kutambua sifa za mfanyakazi wa kigeni kutarahisishwa.
Ujerumani inahitaji wahandisi katika fani ya umeme, wataalamu katika sekta ya vyuma, upishi, uuguzi, huduma za wazee na fani ya kopyuta.