Pole kwa kusubiri! ajirazenu hazitamaliza wiki 2 kutoka sasa, ila jua yafuatayo;-
1. Seckta unayoililia ni sekta ambayo haiitaji haraka kupata maendeleo hata ajira yake haina haraka! endelea kusubiri!
2. Jua 80 percent ya mtakao ajiliwa miezi mtatu ya kwanza haina mshahara, utaanza kwa kuidai serikali so jipange!
3. Vituo vya mjini vyote vimejaa 75 percent wote tumewapanga vijijini na madiwani wametusaidia kwa hilo!
4. Pesa ya kujikimu wala ya mizigo kwa baadhi ya wilaya haitokuwepo so usitarajie makubwa! jipange
5. Shule nyingi hazina nyumba za kutosha, wakuu wa shule wata wasaidieni kwa muda ila jiandae kutangazwa shida zako! Kwa kuwaomba wakuu hao washule msaada!
6. Kumbuka una garantee yakufanya kazi hata kwa miezi 8 bila mshahara toka uanze kazi! jipange
7. Diwani wa kata ndiye bosi wako, hata mkurugenzi wa halmashauri ambaye ndiye mwajiri hana sauti juu ya diwani! Jipange
8. Usipokua makini Utamaliza mwaka kazini na madeni kuliko kipato, kwani kwakuwa hakutakuwa na mshahara basi utakopeshwa na shule uliyopangiwa na baadda ya hapo kama hutopata tena mshahara basi itabidi uwekaribu na mangi akusajili kunako daftarilake! na hata ukija pata mshahara wako kulipwa ule mwingine ni mpaka ustaafu! jipange
9. Kwakuwa utapangiwa kijijini, kumbuka huko hakuna cha tution wala cha semina wala cha mitihani ya kujipima, hii ni kutokana na kuwa wazazi wengi wa vijijini hawana uwezo wakulipia hizo tution, hivyo njia pekee jiandae kisaikolojia kuwa mkulima baada ya vipindi jambo ambalo nila msingi kama utajipanga lita kufanya kuja kusahau shida kama utalifanyia kazi kwa kina!
10. Hakuna maisha rahisi, najua kwa sasa unawaza ukishaipata kazi basi mambo yote yatakuwa safi! kuna changamoto nyingi sana katika maisha ya kada hii! unachopaswa kufanya ni kujipanga kuliko kukaa ungefanya utaratibu wa kujiajili au kujiegesha private ili ukusanye kiasi kitakacho kusaidia kuishi kwa kipindi kifupi kigumu kijacho!
MAMBO SIMARAHISI KAMA MNAVYO DHANIA: UKITAKA KUJUA UTAMU WA MAJI YAVULIE NGUO UYA ONJE: Naomba kuwasilisha. Mwenye la kuongezea ruksa tu