Ajira za walimu 2014

Ajira za walimu 2014

Tafuta ishu za kufanya wakati unasubiri post
wizara ya elimu haina calender siku mulugo akishiba maandazi atatangaza..!

Je mulugo yupo Wizara/Idara gani vile? Ikiwa kama kijiji chako hakina mawasiliano na vijiji vingine, naomba usijibu kwa kuwa utawaaibisha wazee wako.
 
Kuwa na subira tu Mulugo aliondoka na flash disk yenye majina yenu, tumeagiza mtu amfuate songwe akiileta tuna upload hata kesho kutwa. Ikipotea itabidi tuanze upya kupanga. Pia yakiwa yameliwa virus/trojen horse itabidi yapangwe upya. Hazina hapakuwa na fungu ndicho kitu kilicho kuwa kinachelewesha pia.
Are you a Great Thinker too?
 
Mkija huku muanze kutusumbua mnapangiwa vituo mnakimbia
 
Ushauri kidogo tu mwl. mtarajiwa. Leo ni january, weye tayari umeshachoka kusubiri matangazo ya serekali kuhusu ajira. Mbona haraka sana weye?
Tulia tu. Hata wacheleweshe vipi, kuna siku watatangaza tu na jina lako litakuwepo. Ushauri, tafuta kitu cha kufanya wakati unangojea. Jifunze hata somo fulani uweze kulimasta unachoona kitakusaidia uwe masta kwenye somo fulani unalotegemea kwenda kufundisha hao wanafunzi. Ni ushauri tu
 
Kama unaona tabu kusubiri serikalini kuna shule za private zinahitaji waalimu, nenda huko.
 
Pole kwa kusubiri! ajirazenu hazitamaliza wiki 2 kutoka sasa, ila jua yafuatayo;-

1. Seckta unayoililia ni sekta ambayo haiitaji haraka kupata maendeleo hata ajira yake haina haraka! endelea kusubiri!
2. Jua 80 percent ya mtakao ajiliwa miezi mtatu ya kwanza haina mshahara, utaanza kwa kuidai serikali so jipange!
3. Vituo vya mjini vyote vimejaa 75 percent wote tumewapanga vijijini na madiwani wametusaidia kwa hilo!
4. Pesa ya kujikimu wala ya mizigo kwa baadhi ya wilaya haitokuwepo so usitarajie makubwa! jipange
5. Shule nyingi hazina nyumba za kutosha, wakuu wa shule wata wasaidieni kwa muda ila jiandae kutangazwa shida zako! Kwa kuwaomba wakuu hao washule msaada!

6. Kumbuka una garantee yakufanya kazi hata kwa miezi 8 bila mshahara toka uanze kazi! jipange
7. Diwani wa kata ndiye bosi wako, hata mkurugenzi wa halmashauri ambaye ndiye mwajiri hana sauti juu ya diwani! Jipange

8. Usipokua makini Utamaliza mwaka kazini na madeni kuliko kipato, kwani kwakuwa hakutakuwa na mshahara basi utakopeshwa na shule uliyopangiwa na baadda ya hapo kama hutopata tena mshahara basi itabidi uwekaribu na mangi akusajili kunako daftarilake! na hata ukija pata mshahara wako kulipwa ule mwingine ni mpaka ustaafu! jipange

9. Kwakuwa utapangiwa kijijini, kumbuka huko hakuna cha tution wala cha semina wala cha mitihani ya kujipima, hii ni kutokana na kuwa wazazi wengi wa vijijini hawana uwezo wakulipia hizo tution, hivyo njia pekee jiandae kisaikolojia kuwa mkulima baada ya vipindi jambo ambalo nila msingi kama utajipanga lita kufanya kuja kusahau shida kama utalifanyia kazi kwa kina!

10. Hakuna maisha rahisi, najua kwa sasa unawaza ukishaipata kazi basi mambo yote yatakuwa safi! kuna changamoto nyingi sana katika maisha ya kada hii! unachopaswa kufanya ni kujipanga kuliko kukaa ungefanya utaratibu wa kujiajili au kujiegesha private ili ukusanye kiasi kitakacho kusaidia kuishi kwa kipindi kifupi kigumu kijacho!

MAMBO SIMARAHISI KAMA MNAVYO DHANIA: UKITAKA KUJUA UTAMU WA MAJI YAVULIE NGUO UYA ONJE: Naomba kuwasilisha. Mwenye la kuongezea ruksa tu
 
OK! I understand your need. But don't call yourself as mwalomu mtarajiwa. You went school, you got education and at last you got your certificate. Wewe ni Mwalimu by proffetional. Masomo gani unafundisha? Pia kama Bookiping name Commerce in a panda wasiliana name mimi. Luna kazi ya lufundisha O- level students.
 
vipi hiyo chance ntapata kwa GEOG?
 
Pole kwa kusubiri! ajirazenu hazitamaliza wiki 2 kutoka sasa, ila jua yafuatayo;-

1. Seckta unayoililia ni sekta ambayo haiitaji haraka kupata maendeleo hata ajira yake haina haraka! endelea kusubiri!
2. Jua 80 percent ya mtakao ajiliwa miezi mtatu ya kwanza haina mshahara, utaanza kwa kuidai serikali so jipange!
3. Vituo vya mjini vyote vimejaa 75 percent wote tumewapanga vijijini na madiwani wametusaidia kwa hilo!
4. Pesa ya kujikimu wala ya mizigo kwa baadhi ya wilaya haitokuwepo so usitarajie makubwa! jipange
5. Shule nyingi hazina nyumba za kutosha, wakuu wa shule wata wasaidieni kwa muda ila jiandae kutangazwa shida zako! Kwa kuwaomba wakuu hao washule msaada!

6. Kumbuka una garantee yakufanya kazi hata kwa miezi 8 bila mshahara toka uanze kazi! jipange
7. Diwani wa kata ndiye bosi wako, hata mkurugenzi wa halmashauri ambaye ndiye mwajiri hana sauti juu ya diwani! Jipange

8. Usipokua makini Utamaliza mwaka kazini na madeni kuliko kipato, kwani kwakuwa hakutakuwa na mshahara basi utakopeshwa na shule uliyopangiwa na baadda ya hapo kama hutopata tena mshahara basi itabidi uwekaribu na mangi akusajili kunako daftarilake! na hata ukija pata mshahara wako kulipwa ule mwingine ni mpaka ustaafu! jipange

9. Kwakuwa utapangiwa kijijini, kumbuka huko hakuna cha tution wala cha semina wala cha mitihani ya kujipima, hii ni kutokana na kuwa wazazi wengi wa vijijini hawana uwezo wakulipia hizo tution, hivyo njia pekee jiandae kisaikolojia kuwa mkulima baada ya vipindi jambo ambalo nila msingi kama utajipanga lita kufanya kuja kusahau shida kama utalifanyia kazi kwa kina!

10. Hakuna maisha rahisi, najua kwa sasa unawaza ukishaipata kazi basi mambo yote yatakuwa safi! kuna changamoto nyingi sana katika maisha ya kada hii! unachopaswa kufanya ni kujipanga kuliko kukaa ungefanya utaratibu wa kujiajili au kujiegesha private ili ukusanye kiasi kitakacho kusaidia kuishi kwa kipindi kifupi kigumu kijacho!

MAMBO SIMARAHISI KAMA MNAVYO DHANIA: UKITAKA KUJUA UTAMU WA MAJI YAVULIE NGUO UYA ONJE: Naomba kuwasilisha. Mwenye la kuongezea ruksa tu

Huo ni uchochezi( hate speeches).
 
Back
Top Bottom