Ajira za walimu wapya 2014 zatangazwa

Ajira za walimu wapya 2014 zatangazwa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2013/14

Jumla ya Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) ifikapo tarehe 01 Aprili 2014. Kati ya idadi hiyo walimu wa ngazi ya Cheti (Daraja III A) ambao hufundisha katika shule za Msingi ni 17,928 na walimu wa shule za sekondari ni 18,093 (wakiwemo 5,416 wa Stashahada na 12,677 wenye shahada).

Orodha rasmi ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali walikopangwa itatangazwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (PMORALG | Prime Minister's Office - Regional Administration and Local Government) na ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training) ifikapo tarehe 15 Machi, 2014.

Walimu wote wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye Halmashauri walikopangiwa ifikapo tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi mara moja.

Inasisitizwa kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za kiutumishi zifanyiwe kazi na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili kuwawezesha kupata mshahara mwezi Aprili 2014 na hivyo kuepuka ulimbikizaji wa mshahara kwa watumishi wapya wanaoanza ajira.

Mwalimu yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila sababu za msingi zinazokubalika kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi hiyo.

Ikumbukwe kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri umezingatia uwepo wa mahitaji ya walimu. Vile vile, fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba na nauli ambazo zitalipwa kwa kila mwalimu atakayeripoti kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali zimetumwa kwenye Halmashauri walikopangwa walimu hao. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kwenda kuripoti katika Halmashauri alikopangwa.

Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya kufanya kazi walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho baada ya mwalimu kutimiza vigezo na masharti ya uhamisho.

Ni vema ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya. Walimu ambao tayari ni watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na hivi sasa wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao na kuendelea na kazi.

IMETOLEWA NA

JUMANNE A. SAGINI KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI

Thank you
 
Huyu jamaa ni mwongo asilimia zote. Nimesurf kote anakosema wala hakuna jipya. Ni mtu anayetaka attention za waalimu na kuwafanya wajisikie furaha wakati maharage yamekwisha ungua.
 
mvivu wa kufikiri huyo achana nae... na link kawekewa ila bd haoni... kweli mtaani kugumu
 
mkafanya kazi sasa nyie vijana maana mmelia sana humu ndani
 
Huyu jamaa ni mwongo asilimia zote. Nimesurf kote anakosema wala hakuna jipya. Ni mtu anayetaka attention za waalimu na kuwafanya wajisikie furaha wakati maharage yamekwisha ungua.

Ingia website ya TAMISEMI utakuta hii taarifa ni ya kweli
 
Huyu jamaa ni mwongo asilimia zote. Nimesurf kote anakosema wala hakuna jipya. Ni mtu anayetaka attention za waalimu na kuwafanya wajisikie furaha wakati maharage yamekwisha ungua.

unamuita mwenzako muongo hali ya kua wewe ndo muongo namba moja...hivi umeingia kwenye website ya tamisemi na hujaona hiyo taarifa au una makengeza mkuu?.
 
unamuita mwenzako muongo hali ya kua wewe ndo muongo namba moja...hivi umeingia kwenye website ya tamisemi na hujaona hiyo taarifa au una makengeza mkuu?.

Kwa kweli nimeingia na sijaona kitu. Kwani wewe umeona? Mbona ni outdated issue zimejaa?
 
haya haya ajira hiyo mliyokuwa mnaisubilia kwa hamu. cha msingi ni kuchapa kazi.
 
Kwa kweli nimeingia na sijaona kitu. Kwani wewe umeona? Mbona ni outdated issue zimejaa?

Mkubwa baada ya kuniumbua nimerudi tena kwa makini na nimeona Headline lakini simu ikagoma kulifungua hilo file. Nikitoka kazini saa tano nitapitia cafe nifungue. Ila ni kweli. Nirudi nchini nikajipange.
 
Huyu jamaa ni mwongo asilimia zote. Nimesurf kote anakosema wala hakuna jipya. Ni mtu anayetaka attention za waalimu na kuwafanya wajisikie furaha wakati maharage yamekwisha ungua.

Mkuu kwanza sitaki uniombe radhi,pili mimi sio mtoto mdogo nilete uongo kwwnye habari amabyo inagusa maisha ya watu, hii habari ni ya kweli,na ndio maana ukiangalia post yangu imekupa maelezo ya kutosha sana, tembelea web ya TAMISEMI utakiona ninacho kuambia
Ahsante
 
kwanini waseme wametangaza wakati kumbe wana tarajia kutangaza?mmmh
 
Back
Top Bottom